Na Greyson Mwase, Singida

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ameuagiza Mgodi wa Dhahabu wa Shanta uliopo katika wilaya ya Ikungi mkoani Singida kuhakikisha unatoa taarifa za tafiti zake zilizofanyika katika maeneo mbalimbali ili wachimbaji wadogo waweze kuzitumia katika kubaini madini yaliyopo na kuanza kuchimba kwa kufuata sheria na kanuni za madini.

Naibu Waziri Biteko alitoa agizo hilo leo tarehe 19 Novemba 2018 kwenye mkutano wa hadhara na wachimbaji wadogo wa madini uliofanyika katika tarafa ya Mang’onyi wilayani Ikungi mkoani Singida kama sehemu ya ziara yake katika mkoa huo yenye lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wachimbaji wa madini

Aliongeza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Madini imeweka mazingira bora ya uchimbaji wa madini kwa wachimbaji wadogo ikiwa ni pamoja na kuwapatia taarifa mbalimbali za utafiti zilizofanywa na Wakala wa Utafiti na Jiolojia Tanzania (GST) na kampuni za utafiti wa madini lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa uchimbaji wao unakuwa wa uhakika na sio wa kubahatisha.

Akielezea maboresho mengine yaliyofanywa katika sekta ya madini, Biteko alisema Serikali imeboresha Sheria ya Madini inayotambua madini kama mali ya watanzania yanayosimamiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.Aliendelea kusema kuwa, Serikali imeweka mkakati wa kurasimisha wachimbaji wadogo wa madini wasio rasmi na kuwapatia leseni za madini ili uchimbaji wao ulete tija kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi.

Meneja Mkuu wa kampuni inayojishughulisha na uchimbaji wa madini ya jasi ya General Business and Equipment Supply Limited iliyopo katika eneo la Bumbua wilayani Itigi mkoani Singida, Yusuph Kibira (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (katikati) mara alipofanya ziara katika eneo la mgodi huo.
Sehemu ya wachimbaji wadogo wa madini wakiwasilisha kero mbalimbali mbele ya Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (hayupo pichani) kwenye mkutano wa hadhara wa wachimbaji wadogo wa madini uliofanyika katika tarafa ya Mang’onyi iliyopo wilayani Ikungi mkoani Singida.
Kutoka kulia, Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Mtaturu walisikiliza kero mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa na wachimbaji wadogo kutoka katika tarafa ya Mang’onyi iliyopo wilayani Ikungi mkoani Singida kwenye mkutano wa hadhara. (hawapo pichani).
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Mtaturu akifafanua jambo kwenye mkutano wa hadhara wa wachimbaji wadogo wa madini uliofanyika katika tarafa ya Mang’onyi iliyopo wilayani Ikungi mkoani Singida.

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko akielezea mikakati ya Wizara ya Madini katika kuboresha shughuli za uchimbaji mdogo wa madini kwenye mkutano wa hadhara wa wachimbaji wadogo wa madini uliofanyika katika tarafa ya Mang’onyi iliyopo wilayani Ikungi mkoani Singida.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...