Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

 MKURUGEZI wa Utangazaji Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Frederick Ntobi amewaasa vijana kutumia fursa za kiteknolojia za kisasa kubuni vitu mbalimbali vitakavyosaidia maendeleo ya  kiuchumi.

Akizungumza katika Maonesho ya Mawasiliano yaliyofanyika viwanja vya Posta, Ntobi amesema teknolojia za kisasa zikitumiwa vizuri zinaweza kubadili kubadili mwenendo wa uendeshaji wa shughuli za kiuchumi nchini.

Amesema  maonyesho ya kwanza ya Mawasiliano yaliyoandaliwa na Kampuni ya Aecco Cunsulting kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Kitivo cha Tehama jiji hapa.Amesema Maonesho hayo yanalenga kukuza biashara na kuongeza mwanya wa ubunifu na kukuza uchumi wa viwanda nchini.

"Maonesho haya yatasaidia vijana kujitangaza lakini  wabadilike kutoka matumizi ya Tehama ya kuwasiliana mambo ya hovyo na badala yake watumie mawasiliano yenye tija ili kuibua ajira na kukuza uchumi wa mtu mmoja moja na hatimaye uchumi kwa taifa" amesema Ntobi

Ntobi TCRA inahimiza kampuni zote za sekta ya mawasiliano kutoa fursa kwa vijana kupata mafunzo kazini ili wawe wabobezi katika masuala ya Tehama.Ubunifu wa vijana wetu wakiwa katika kampuni  unaweza kuleta maendeleo katika sekta ya mawasiliano kwani sasa tunakwenda  kwenye uchumi wa  viwanda hivyo vinahitaji rasilimali watu wenye ujuzi wa kuendesha mitambo kwa njia ya teknolojia ya kisasa"amesemaNtobi.

Ntobi ametoa rai kwa watoaji mafunzo katika katika vyou kuwa elimu na maarifa wanayotoa kwa wanafunzi  iwe chachu ya kujenga uwezo na ubunifu katika utendaji wa maisha yao.Naye Meneja Mradi wa Aecco Jacqueline Buretta amesema wanatambua mchango wa mawasiliano katika kukuza uchumi wa viwanda hivyo maonyesho hayo ni muhimu na yako katika muda mwafaka

"Nia yetu ni kuendeleza ushirikiano na wadau wa sekta ya mawasiliani katika kuhakikisha kuwa na nafasi ya kuonesha bidhaa za mawasiliano kwa nia yabkuonesha umma upana wa sekta ya mawasiliano," Hata hivyo amesema Maaendeleo ya ubunifu katika sekta ya mawasiliano haitofanikiwa bila ushuriki wa vyuo vikuu.
 Picha ya pamoja.
 Mkuu wa Chuo, Ndaki ya Tehama Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Dkt. Mussa Kissaka akizungumza kuhusiana na utoaji wa elimu katika Chuo hicho katika masuala ya Tehama.
 Meneja wa Mardi AECCO na Waandaji wa maonesho Jucqline Buretta akizungumza kuhusiana na maonesho yaliyofanyika Jijini Dar Salaam.
 Mkurugenzi wa Utangazaji wa TCRA, Fredrick Ntobi na Afisa Mwandamizi wa Mahusiano na Mawasiliano Mabe Masasi wakiwakabidhi muongozo wadau wa mawasiliano.
Mkurugenzi wa Utangazaji wa TCRA Fredrick Ntobi akizungumza wakati akifungua Maonesho ya Mawasiliano yaliyofanyika katika viwanja vya Posta jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...