Na Ahmed Mahmoud Arusha
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania(TCRA)imewataka wale wote wenye kuuza bidhaa za mawasiliano ikiwemo simu za mkononi,Radio na Runinga kuhakikisha wanajisajili kwao ili wananchi wapate huduma zilizo sahihi na kuondoa malalamiko kutopata huduma stahiki

Akizungumza kwenye semina ya huduma za utangazaji kwa channeli zinazotazamwa bila malipo iliyowashirikisha watendaji wa mitaa,Kata, Wakuu wa vituo vya polisi,waalimu wakuu wa shule sanjari na watumisha wa idara za serikali wilayani hapa Meneja wa mamlaka hiyo Mhandisi Fransis Msungu amesema kuwa hapa Arusha mamlaka hiyo imebaini kuwa wafanyabiashara wengi wana leseni za biashara lakini za mamlaka hiyo wengi wao hawana.

Amesema kuwa maswali mengi yalioelekezwa kwa mamlaka hiyo imeonyesha mafundi wa simu na maduka mengi hayana leseni za mamlaka hiyo hivyo kutoa wito kwao kuangalia na kujisajili haraka kwao ili kuweza kumlinda mlaji.

“Nawasihi wote kuhakikisha wanajisajili haraka kwao ili kuwezakuondoa malalamiko yanayotolewa na walaji kwa mamlaka yetu utaona hapa Arusha kuna maduka 40 yenye leseni zetu mengi yaliopo bado hayajasajiliwa sanjari na mafundi wa simu”alitanabaisha Msungu.

Kwa Upande wake Katibu Tawala wa wilaya ya Arusha David Mwakiposa amesema kuwa mbali na malalamiko mbali mbali yaliotolewa na washiriki wa mkutano huo suala zima ni mashirikiano kati ya Tcra na wadau mbalimbali na semina hiyo imefungua milango kwa wananchi kwani elimu itawafikia walengwa ambao ni wananchi.
 Meneja wa TCRA Kanda ya Kaskazini Fransis Msungu akiongea kwenye semina iliyowashirikisha watendaji wa kata na mitaa waalimu wakuu kutoka halmashauri za jiji na wilaya ya Arusha sanajri na wakuu wa vituo vya polisi wilayani hapa iliyofanyika kwenye hotel ya Golden Rose jijini hapa.
 Muwasilishaji kutoka mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA Janny Kaaya akitoa mada wakati wa semina ya watendaji wa kata na mitaa waalimu wakuu na wakuu wa vituo vya polisi walioshiriki semina hiyo kwenye hotel ya Golden Rose jijini hapa.
Katibu tawala wa wilaya ya Arusha mjini David Mwakiposa akifunga semina hiyo iliyowashirikisha Halmashauri za jiji la Arusha na wilaya ya Arusha iliyofanyika kwenye Hoteli ya Golden Rose jijini hapa picha na mahmoud ahmad wa globu ya jamii Arusha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...