Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo, Mtwara

Ikiwa ni siku moja tu mara baada ya kuapishwa kuongoza wizara ya kilimo katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam Jana Jumatatu Novemba 12, 2018, Waziri wa kilimo Mhe Japhet Ngailonga Hasunga (Mb) Leo Tarehe 13 Novemba 2018 ameongoza viongozi wakuu wa Wizara yake kutembelea katika Mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma kwa ajili ya kuhakiki Korosho zilizopo katika maghala makuu.

Katika msafara huo Waziri Hasunga atatembelea Mkoani Mtwara ambapo ameambatana na Naibu Waziri wa kilimo Mhe Innocent Lugha Bashungwa na Katibu Mkuu Mhandisi Mathew Mtigumwe watakaotembelea Mkoa wa Lindi, na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Prof Siza Tumbo atakayetembelea Mkoa wa Ruvuma.

Katika ziara hiyo viongozi hao wakuu watahakiki usimamizi wa maghala ambao kwa sasa unasimamiwa naBodi ya usimamizi wa stakabadhi ya ghala na Usimamizi wa ziada wa Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Bodi ya Nafaka na Mazao mchanganyiko.

Vilevile watahakiki taarifa za Ubora wa maghala kama zilivyopitishwa na Bodi ya usimamizi wa Stakabadhi ya ghala (Warehouse Receipt Regulatory Board-WRRB) pamoja na Ubora wa ghala.Watahakiki uwezo wa maghala na kiasi kilichopo ghalani, na kuhakikisha taarifa ya umiliki wa Korosho zilizopo kwenye ghala.

Aidha, viongozi hao watahakiki kiasi cha Korosho kwenye ghala kwa kupitia nyaraka za mapokezi ya Korosho kwenye ghala ambazo zinawasilishwa na Vyama vya msingi (AMCOS) na kuoanisha taarifa hizo na taarifa zilizomo kwenye taarifa za stakabadhi ya ghala (Warehouse Report).

Katika ziara hiyo timu ya viongozi wakuu kutoka wizara ya kilimo wataambatana pia na Ofisini za Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Bodi ya Mazao Mchanganyiko, Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania (TARI)-Naliendele, na Bodi ya usimamizi wa Stakabadhi ya ghala (WRRB).
Waziri wa kilimo Mhe Japhet Ngailonga Hasunga (Mb) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe Evod Mmanda leo Novemba 13, 2018 mara baada ya kuwasili Mkoani humo kwa ziara ya kikazi kwa ajili ya kuhakiki Korosho zilizopo katika maghala makuu kabla ya kuanza ununuzi. (Picha Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo)
Waziri wa kilimo Mhe Japhet Ngailonga Hasunga (Mb) akijadili jambo na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe Gelasius Byakanwa leo Novemba 13, 2018, mara baada ya kuwasili Mkoani humo kwa ziara ya kikazi kwa ajili ya kuhakiki Korosho zilizopo katika maghala makuu kabla ya kuanza ununuzi.
Naibu waziri wa kilimo Mhe Innocent Lugha Bashungwa (Mb) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi kwa ajili ya kuhakikisha Korosho zilizopo katika maghala makuu kabla ya kuanza ununuzi. Mwingine pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe Evod Mmanda, leo Novemba 13, 2018.
Kulia ni katibu Mkuu wa wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe na Naibu Katibu Mkuu wizara ya kilimo Prof Siza Tumbo walipowasili Mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi kwa ajili ya kuhakikisha Korosho zilizopo katika maghala makuu kabla ya kuanza ununuzi leo Novemba 13, 2018.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...