Na Khadija Seif,Globu ya jamii

SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC) limesema linajivunia kuboresha miundombinu ya reli nchini ikiwa ni mkakati wa kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Magufuli kuboresha miundombinu hiyo ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa Standard Gauge Railways (SGR).

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Masanja Kadogosa wakati anazungumzia miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais Dk.John Magufuli ambapo amesema shirika hilo lina majukumu ya kutoa huduma za usafiri wa abiria wa treni za mikoani na treni za mizigo ndani ya nchi na nje.

Pia amesma kwa sasa TRC imerudisha safari ya treni ya mizigo kutoka Dar es salaam mpaka Mji wa Kampala nchini Uganda, ambapo ikiwa na miradi miwili ambayo ni mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) na mradi wa uboreshaji wa reli ya kati pamoja na miradi midogo kama kurejesha njia ya Tanga, Arusha na Moshi na baadae Mtwara,Mbambabei na njia ya Singida.

Kadogosa amefafanua zaidi kuwa mapato yameongezeka kutokana na huduma zinazotolewa na TRC na kuboreshwa kwa huduma za shirika hilo kwa mwaka 2017/2018 na kufikia kiasi cha Sh.bilioni 36 tofauti na mwaka 2016/2017 ambapo kiasi cha fedha kilikua Sh. bilioni 23.

Pia amesema kuna miradi ya ujenzi wa miundombinu ya reli inaendelea kutekelezwa katika sehemu mbili za mwanzo zinazojumuisha Dar es salaam na Makutopora, kwa lengo la ifikapo 2021 Aprili , sehemu hizo mbili za mradi ziwe zimekamilika. Pia amesema katika ujenzi huo TRC limetoa zabuni kwa wakandarasi ambao ni ubia wa kampuni ya Yapi Merkezi kutoka nchi ya Uturuki na Mota Engil kutoka nchini Ureno.

Wakati huo huo amesema kuna Kampuni za wazawa 16 zinazoshiriki katika ujenzi wa reli ya kisasa kama Wakandarasi,Wasambazaji wa bidhaa na watoa huduma, lengo likiwa ni kushirikiana kati ya wazawa na wageni katika kujifunza na kujiongezea ufanisi mkubwa ili kuleta maendeleo kwenye nchini yetu hususani Kwenye usafiri wa treni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...