Naibu Waziri Wizara ya Kilimo Mhe. Omary Mgumba ameitaka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ishirikiane na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali na wataalam kutoka chuo kikuu cha ardhi kuhakiki eneo lenye ukubwa wa hekta 475,052 liloripotiwa na Tume hiyo kuwa linafaa kwa kilimo cha Umwagiaji nchini. 

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe. Mgumba ameyasema hayo alipofanya ziara katika ofisi za Tume Jijini Dar es Salaam ili kuongea na watumishi, ambapo aliwataka wao kama Tume washiriki kwanza kuhakiki eneo hilo na kuweza kutoa taarifa za uhakika. 

“Mnaweza kushirikiana na ofisi za kanda na halmashauri ili kuweza kurahisisha kufanyika kwa kazi hii , kwenye kilimo ni vyema tukaenda na mambo yote matatu, kilimo cha kutegemea maji ya mvua, kiimo cha kutegemea maji ya ardhini na kilimo cha kisasa cha umwagiliaji cha kutumia miundombinu, kilimo ambacho kitatuhakikishia uhakika wa chakula kwani ni kilimo ambacho mkulima analima zaidi ya mara moja kwa mwaka.” Alisema Naibu Waziri. 

Sambamba na hilo, Naibu Waziri ameitaka Tume pia kuwasilisha kwake taarifa ya utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi katika eneo la kilimo cha umwagiliaji kwa kipindi cha miaka mitatu ya serikali ya awamu ya tano na taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali. 

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe. Omary Mgumba akizungumza na watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, wakionekana baadhi katika picha jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri Wizara ya Kilimo Mhe. Omary Mgumba akiongea na watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji wa Miundombimu ya Umwagiliaji Mhandishi Pascal Shayo, kulia ni katibu wa TUGHE tawi la Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Cretus Mbogo
Baadhi ya watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji katika kikao na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Omary Mgumba jijini kilichofanyika jijini Dar es Salaam leo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...