Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii,Newala ,Mtwara.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Newala, Mussa Chimae amesema tangu kutangazwa kwa operesheni korosho ofisi yake kwa kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Newala wamezunguka  Wilaya nzima kutoa elimu kuhusu nini kifanyike kupitia agizo la Rais Magufuli kuwa Serikali itanunua Korosho yote nchini.

Akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo ofisini kwake Wilayani Newala Chimae amesema kuwa  wamezunguka kwa wananchi kutoa elimu juu ya namna zoezi hilo litakavyoendesha ikiwa ni pamoja na kuwataka watendaji wa vijiji na kata kusimamia zoezi hilo kwa makini hili kusitokee malalamiko yoyote.
"Sambamba na zoezi la uhakiki wa taarifa za wakulima pia tumetoa maagizo kwa watendaji wa mitaa na kata kusimamia zoezi la uingizaji wa korosho kwenye maghala na kuhakikisha kuwa hakuna korosho inayoingia kutoka nje ya mitaa au kata zao ili kudhibiti korosho za magendo zinazoingizwa kutoka nchi jirani," alisema Chimae.

amesema kuwa Halmashauri ya Newala ni moja ya Halmashauri zinazopakana na nchi jirani ya Msumbiji ambapo kwa upande wa majirani zetu kwa sehemu nao wanalima zao la Korosho hivyo wamejipanga kwa kila namna kwa kushirikiana na Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) Kuwa hakuna korosho kutoka nchi jirani itakayopenya nchini kupitia milango ya Wilaya hiyo.

amesema kuwa tayari askari wa JWTZ Wamejipanga katika Maghala na wameimarisha ulinzi kwa kukagua na kulinda korosho hili isije mtu akatokea akatia doa wilaya yake kwa kufanya vitu tofauti na maagizo ya Rais.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Newala, Mussa Chimae akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu  Mafanikio yaliyopatikana katika Wilaya hiyo kwa kipindi hiki cha Miaka Mitatu ya Serikali ya  awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli

Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya Habari wakimsikiliza
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Newala, Mussa Chimae
Jengo la Utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Newala linavyoonekana kwa nje

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...