Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa
Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle kulia akijadiliana jambo na
Meneja wa kampuni ya Kizalendo ya Songoro Marine Boatyard ya jijini Mwanza
Major Songoro mara baada ya kukagua kivuko cha MV. Chato ambacho ukarabati wake
umemalizika, kivuko hicho chenye uwezo wa kubeba tani 75 sawa na abiria 200,na
magari 6 kinatoa huduma Wilaya ya Chato, maeneo ya Ikumba Itale, Izumacheli,
Muharamba, Senga, Bukondo na Bwina Mkoani Geita .
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa
Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle wa pili kulia akisisitiza
jambo kwa Meneja wa kampuni ya Kizalendo ya Songoro Marine Boatyard Major
Songoro wa pili kushoto mara baada ya kukagua kivuko cha MV. Chato ambacho
ukarabati wake umemalizika, tukio lililofanyika katika yadi ya Songoro iliyopo
Ilemela mjini Mwanza. Kivuko hicho cha tani 75 kina uwezo wa kubeba abiria 200 na
magari 6 na kinatoa huduma katika Wilaya ya Chato, maeneo ya Ikumba Itale,
Izumacheli, Muharamba, Senga, Bukondo na Bwina Mkoani Geita. Kushoto ni Mkurugenzi
Huduma za Ufundi (WUUM) Mhandisi Lazaro Vazuri na kulia ni Meneja wa TEMESA
mkoa wa Mwanza Mhandisi Hassan Karonda.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa
Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle (aliyevaa suti) akizungumza
na waandishi wa habari mara baada ya kukagua kivuko cha MV. Chato ambacho
ukarabati wake umemalizika, tukio lililofanyika katika yadi ya Songoro mjini
Ilemela Mwanza. Kivuko hicho cha tani 75 kina uwezo wa kubeba abiria 200 na
magari 6 na kinatoa huduma katika Wilaya ya Chato, maeneo ya Ikumba Itale,
Izumacheli, Muharamba, Senga, Bukondo na Bwina Mkoani Geita.
Muonekano wa kivuko cha MV. Chato
mara baada ya kukamilika kwa ukarabati wake. Kivuko hicho cha tani 75 kina
uwezo wa kubeba abiria 200 na magari 6 kinatarajiwa kurudishwa katika kituo
chake kuendelea na kazi ya kuvusha abiria maeneo ya Ikumba Itale, Izumacherl,
Muharamba, Senga, Bukondo na Bwina Mkoani Geita.
Kivuko cha MV. Chato kikielea
majini baada ya kukamilika kwa ukarabati wake ambao. Kivuko hicho cha tani 75
kina uwezo wa kubeba abiria 200 na magari 6 kinatarajiwa kurudishwa katika
kituo chake Wilayani Chato Mkoani Geita
kuendelea na kazi ya kuvusha abiria.
PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO (TEMESA)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...