Na Dotto Mwaibale, Mtwara

IMEELEZWA kuwa upatikanaji wa dawa vifaa tiba na vitendanishi vya maabara mkoani Mtwara ni asilimia 97 ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo ilikuwa chini ya asilimia 40.

Hayo yamebainishwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara, Jully Maleko, wakati akizungumza na waandishi wa habari na maofisa wa Bohari ya Dawa (MSD) ambao wapo mkoani humo kuwatembea wateja wao na kujua changamoto walizonazo ili kuzifanyia maboresho.

"Hivi sasa hali ya upatikaji wa dawa katika mkoa wetu ni nzuri tumefikia asilimia 97 ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo tulikuwa chini ya asilimia 40" alisema.Mfamasia wa Hospitali ya Mkoa ya Mtwara Ligula, Boniface Magige alisema changamoto kubwa waliyonayo ni ukusanyaji wa fedha vituoni baada ya kupelekewa dawa pamoja na kada ya wafamasia kuwa wachache.

Katika hatua nyingine MSD imetambulisha mfumo wa upatikanaji wa taarifa muhimu kwa wateja wake, ambazo ni pamoja na taarifa za upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara na bei zake, taarifa za akaunti zao na taratibu za maombi ya bidhaa wanazo hitaji kutoka MSD.

Taarifa hizo zinapatikana kwenye mfumo maalum wa kieletroniki unaojulikana kama“MSD-Customer Portal” unaweza kutumika na wateja wake popote walipo nchini na kuwaondolea usumbufu waliokuwa wakiupata awali wakati wakuagiza dawa, ambapo ili walazimu kusafiri ofisi za Kanda ya MSD inayowahudumia au kupiga simu ili kupata taarifa hizo na nyinginezo.
Afisa Huduma kwa Wateja wa Bohari ya Dawa (MSD), Florida Sianga (kushoto), akiwaelekeza Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Naliendele iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani Abdallah Njee (katikati) pamoja na Mtunza Dawa wa Zahanati hiyo, Pili Makota (kulia), jana, mfumo maalum wa kieletroniki unaojulikana kama“MSD-Customer Portal” unaweza kutumika na wateja wake popote walipo nchini jinsi ya kuagiza dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara na bei zake, taarifa za akaunti zao na taratibu za maombi ya bidhaa wanazo hitaji kutoka MSD. Wa pili kutoka kushoto ni Afisa Huduma kwa Wateja wa MSD Mkoa wa Mtwara, Larisa Manyahi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara, Jully Maleko akizungumzia upatikanaji wa dawa katika mkoa huo.
Mganga Mkuu wa Halmshauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani, Joseph Kisala, akizungumzia upatikanaji wa dawa katika halmashauri hiyo.
Muuguzi Msaidizi wa Zahanati ya Kijiji cha Rwelu, Shadida Rashidi (katikati), akimuonesha moja ya kopo lenye dawa Afisa Huduma kwa Wateja wa MSD, Florida Sianga. Kulia ni Mfamasia wa Hospitali ya Mkoa ya Ligula Mtwara, Boniface Magige.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...