Na.Khadija Seif,Globu ya jamii.

Kundi la taarab First class modern taarab linalofanya vizuri kwa sasa linatarajia kufanya uzinduzi wa albam yao ya kwanza tarehe 10 mwezi huu jijini Dar es salaam.

Akizungumza na wadau pamoja na wanahabari Jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa bendi hiyo Aboubakar Soud maarufu kama Prince Amigo amesema kuwa bendi hiyo ilianzishwa rasmi mwaka huu na kuiona fursa ya kutoa burudani yenye hadhi na heshima kwa rika zote. 

Aidha amefafanua ujio wa First Class Modern Taarab ambao umekusanya vijana wengine kutoka bendi kongwe hapa nchini lengo likiwa ni kutoa uhondo wa hadhi.Amigo ameeleza kuwa albam hiyo itazinduliwa rasmi katika ukumbi wa travertine Magomeni na kusindikizwa na wakongwe wa taarab nchini kama sabaha Salum muchacho, Rukia Ramadhani ,Mwanahawa Ally, Mwanamtama Amir pamoja na Patricia Hillary.

Msemaji wa bendi hiyo kwa upande wa matayarisho Haji Mabovu ameeleza kuwa tiketi zinapatikana kwa bei ya kitanzania shilingi elfu tano na getini zinapatikana kwa bei ya shilingi elfu nane. Sanjari na hilo uzinduzi utaambatana na uuzwaji wa albam yao inayobeba jina la Mama wa hiyari ,jezi pamoja na t-shirt lengo ni kuwapatia fursa watu kufaidika na bendi hiyo. 

Amewaomba mashabiki waliokuwa wakitoa ushirikiano wakati alipokua bendi nyingine wajitokeze kutoa ushirikiano Kwenye bendi ya 
First Class Modern Taarab ambapo Amigo ndio Mkurugenzi wa bendi hiyo.
Mkurugenzi wa bendi ya first class modern taarab akitambulisha muonekano wa albam yao ya Kwanza inayokwenda kwa jina la Mama wa hiari itakayozinduliwa rasmi tarehe 10 mwezi huu katika ukumbi wa traventine

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...