Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu yamezinduliwa rasmi tarehe 14 Novemba 2018 huku Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) ikipewa jukumu la kuratibu mchakato wa mashindano katika makundi mawili ambayo ni Wabunifu wa Ufundi Stadi na Wabunifu wa kutoka Sekta Isiyo Rasmi, hivyo kupata majina matano ya kila kundi kuingia kwenye fainali.

Akizindua mashindano hayo sambamba na Mwongozo wa Kuendeleza Ugunduzi, Ubunifu na Maarifa Asilia, kwenye Ukumbi wa Kambarage, Nyerere square jijini Dodoma, Waziri wa sayansi na teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako alisema mashindano hayo yataongozwa na kaulimbiu ya “Kukuza Ujuzi na Ubunifu kwa Uchumi wa Viwanda,” na yatahusisha makundi mbalimbali ya wabunifu wa kisayansi, teknolojia katika maeneo na nyanja mbalimbali nchini kote, ambapo kilele chake kitakuwa Januari 2019.

Alisema ili nchi yetu iweze kunufaika na matokeo ya ubunifu, uvumbuzi na maarifa asilia, kuna umuhimu wa kuwahamasisha wagunduzi, wabunifu na wamiliki wa maarifa asilia.

“Kwa hiyo, mashindano haya yatasaidia kuibua vipaji na kuhamasisha uendelezaji wa teknolojia na ubunifu utakaoweza kuchangia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo endelevu ya viwanda, kuongeza tija ya uzalishaji wa malighafi, kuongeza thamani ya bidhaa zinazozalishwa nchini pamoja na kuboresha shughuli nyingine za kiuchumi. Kutokana na kutambua umuhimu wa sayansi, teknolojia na ubunifu, Wizara yangu ina mpango wa kufanya mashindano haya yafanyike kila mwaka ili uibuaji wa vipaji vya namna hii uwe endelevu,  ” alisema.

Aliongeza kuwa Mwongozo wa Kuendeleza Ugunduzi, Ubunifu na Maarifa Asilia utakuwa ni nyenzo ya kuongeza ufanisi wa taasisi zinazoshughulikia masuala ya ugunduzi, ubunifu na umiliki wa maarifa asilia.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...