Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii, Mtwara

WAZIRI wa Kilimo Japhet Hasunga, amesema serikali imeshaanza uhakiki wa wakulima wanaodai malipo ya korosho ambapo jumla ya vyama vya msingi 35 vimeshahakikiwa na malipo yameanza kufanyika.

Hayo aliyasema jana mkoani Mtwara wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu opereshe korosho inayoendelea katika mikoa inayolima korosho kuhakikisha wakulima wote wanauza korosho zao kwa serikali kwa bei ya Sh. 3,300.

"Tulitenga vyama 50 vya awamu ya kwanza na ndani ya siku mbili tumehakiki taarifa za wakulima kwenye vyama 35 kwa kuangalia majina yao, kiasi cha korosho walichoingiza kiasi cha fedha wanazotakiwa kulipwa na taarifa za akaunti zao na hivi ninavyoongea tayari wameanza kulipwa kuanzia sasa kupitia akaunti zao binafsi," alisema Hasunga.

Alitaja halmashauri ambazo vyama vyao vimehakikiwa kuwa ni pamoja na Halmashauri ya Newala (5) Wilaya ya Newala (5) Wilaya ya Masasi (5) Nanyumbu (2) Lindi (5) Tunduru Ruvuma (5).Kuhusu malipo ya kitaasisi ikiwemo ushuru wa halmashauri alisema inaanda mwongozo wa kuangalia namna ya kuwalipa na kwamba malipo yatafanyika baada ya korosho kubanguliwa na kuuzwa.

"Ili kulipa malipo ya makato yote lazima tujue tumeuza korosho kwa bei gani kisha kama ni asilimia zinakatwa kulinga na bei tuliyouzia," alisisitiza.Makato hayo ya kitaasisi huwa yanalipwa kwa Halmashauri ambayo huchukua asilimia tatu ya bei elekezi, wasafirishaji wa korosho, watunza maghala pamoja na vyama vikuu vya ushirika ambavyo hukata Sh. 53 katika kila kilo moja ya korosho kwaajili ya vifungashio.

Hasunga yupo mikoa ya kusini tangu siku moja tu baada ya kuteuliwa kwenye nafasi hiyo ili kujionea zoezi la uingizaji korosho kwenye maghala na kuhakikisha kuwa hazitoki na kuuzwa baada ya serikali kuweka msimamo wa kununua korosho zote za wakulima nchini.

Alisema kwasababu serikali ndiyo mnunuzi wa korosho hivyo inalazimika kulipa tozo ambazo walikuwa wanalipa wanunuzi wengine."Kwa agizo la Rais fedha zote zitapelekwa kwa wakulima bila makato yoyote kwasababu tunaangalia wakulkma kwanza na wengine watalipwa baadae" alisema.
Waziri wa Kilimo , Japhet Hasunga akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu utaratibu wa kutoa Malipo ya korosho kuanzia leo Novemba 17 mwaka 2018 kama ilivyoagizwa na Rais Dr.John Pombe Magufuli.
Baadhi ya Wanafunzi wakiwa wametoka kuokota korosho katika Mashamba ya shule kwa ajili ya kukusanya ziende kuuzwa kwenye Maghala.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...