Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.
AFISA  Manunuzi  Mwandamizi wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula, Mohamedx Mzingi na Mkuu wa Textile Leather wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na makosa miwili likiwemo la matumizi mabaya ya madaraka na kusababisha hasara ya zaidi ya Sh milioni 977.
Akisoma hati mashtaka wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Aneth Mavika amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Augustina Mmbando kuwa kati ya Julai 16 na 30, mwaka 2013 katika ofisi za Makao Makuu ya Hifadhi ya Chakula (NFRA) washtakiwa walitenda kosa.

Imedaiwa siku ya tukio washtakiwa hao kwa nafasi zao na wakiwa wajumbe wa uthamini wa zabuni walitumia madaraka yao vibaya katika uthamini wa  zabuni namba AE-054/2013/2014/HQ/G/02 Lot namba 01.

Wakili huyo aliendelea kudai kuwa washtakiwa walitenda kosa hilo wakati wakitekeleza majukumu yao ambapo kwa makusudi walipendekeza kampuni ya Bajuka International (T) Ltd ambayo ilikuwa haina sifa kupewa zabuni ambayo haikuendana na matakwa ya kitaalam kama yalivyokuwa kwenye nyaraka za zabuni kitendo ambacho ni kinyume cha sheria.

Pia washtakiwa hao wanadaiwa kushindwa kutimiza majukumu
yao kikamilifu na kuisababishia Wakala wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kupata hasara ya Sh milioni 997, 040,000.

Hata hivyo, washtakiwa wamekana kutenda makosa hayo ambayo wanashtakiwa chini ya sheria ya uhujumu uchumi kwa sababu yaliambatanishwa na kibali cha DPP ambacho kiliipa ridhaa Mahakama hiyo kusikiliza Kesi hiyo na kutoa dhamana.

Hata hivyo washtakiwa wamekana kutenda kosa hilo na upande wa mashtaka umedai  kuwa upelelezi bado haujakamilika.

Akitoamasharti ya dhamana, Hakimu Mmbando alimtaka kila mshtakiwa kuwa na wadhamini Wakili wanaoaminika ambao kila mdhamini asaini bondi yaSh165 milioni huku mmoja kati ya wadhamini hao ametakiwa kuwasilisha hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya kiasi hicho cha Fedha. Pia washtakiwa hao wametakiwa kuwasilisha hati zao za kusafiria mahakamani.

Hata hivyo mshtakiwa Mohammed alikamilisha masharti ya dhamana na kuachiwa huru huku mwenzake Peter alishindwa kuyakamilisha na kupelekwa rumande. Aidha Mahakama imetoa hati ya wito kwa mshtakiwa Edward Mtango ambaye hakuwepo mahakamani wakati wenzake wakisomewa mashtaka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...