KAMPUNI  ya  uchakataji  wa  asili  ya Ruaha farm  mkoani Iringa kupitia asali yake Ruaha  Honey  imeanza  kuwaokoa  kiuchumi  wafugaji wa  nyuki  mkoani Iringa kwa kutoa  mizinga na  kuwaunganisha na  soko la asali .

"kampuni  ya Ruaha Farm  imekuja  kivingine  baada ya  kufunga mashine  za  kisasa  za  kuchakata  asali  yenye  ubora pasipo  kutumia vifaa vya  kienyeji kama moshi  na vingine "
 Mkurugenzi  mtendaji wa kampuni ya Ruaha  Honey  Fuad Abri  alisema  kuwa  kampuni yake  imeendelea  kuunga mkono jitihada za  serikali  ya  awamu ya  tano  chini ya   Rais Dkt  John Magufuli ya Tanzania  ya  viwanda.

 Alisema ubora wa  asali  ya kampuni ya Ruaha Honey  ni tofauti na  asali   nyingine  zinazouzwa  mitaani kwani  sifa  kubwa ya  asali  ya Ruaha honey ni asali halisi toka katika vijiji vinavyozunga hifadhi ya Ruaha national park. Asali ya ruaha honey ni Asali bora inayozingatia usafi wa vyombo, usafi wa uchakatishaji pamoja na ufugaji wa nyuki kwa njia salama na rafiki kwa nyuki.

 Alisema  Ruaha honey ni asali ya kampuni ya ruaha farm pamoja na wafugaji wa nyuki wa vijiji vinavozunguka hifadhi ya ruaha. 

 Kampuni ya Ruaha honey inashirikiana na  wafuga nyuki wa Iringa kwa kuwawezesha kupata mizinga ya kisasa na kupatiwa mafunzo ya mara kwa mara ya ufugaji  sahihi wa nyuki ili kulinda ubora wa mazao ya nyuki yanayopatikana kama asali na nta.

 Ruaha honey pia inawapatia soko la asali wafugaji wa nyuki kwa lengo la kuinua kiuchumi kaya maskini kupitia ufugaji wa nyuki alisema  Abri. Kuwa  asali ya Ruaha ni asali halisi inayotokana na uoto asili wa miti ya Acacia, mibuyu na miti pori na maua pori hivyo  ni asali  bora   zaidi .

 Alisema  kupitia kampuni  ya Ruaha farm inafugia nyuki katika shamba lake liliopo Tungamalenga ambayo ni hifadhi ya nyuki ya kwanza binafsi Tanzania na Afrika mashariki

Lengo ni kuinua ufugaji wa nyuki wa nyanda za juu kusini  pia  kuendeleza  ufugaji wa nyuki  kisasa  kama  sehemu ya  kuwa na  viwanda  bora  vya mazao  yatokanayo na  nyuki .

 Hifadhi  ya nyuki ya Ruaha ni eneo linafanyika    utafiti mbali mbali wa nyuki pamoja na mazao yake, pia ni shamba darasa kwa wafuga nyuki wengine wanaozunguka eneo hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...