*Wawaoma BMT, TFF kuheshimu maamuzi ya mkutano mkuu wa Yanga wa kumtambua Yusuf Manji kama Mwenyekiti wao.

*kuhusu uchaguzi, Mwenyekiti wa Matawi aitwa kamati ya maadili kesho

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

WANACHAMA wa Klabu ya Yanga kwa pamoja wameazimia kuweka msimamo wao wa kutotaka uchaguzi wao kusimamiwa na kamati ya uchaguzi ya TFF na Yusuf Manji bado ni Mwenyekiti wao wanamtambua.

Baraza la Michezo (BMT) wiki iliyopita walitoa tamko la kuwataka TFF washirikiane na Yanga kuhakikisha wanafanya uchaguzi mkuu wa kujaza nafasi zilizokuwa wazi baada ya vionozi wake kijiuzulu na pia kujaza nafasi ya Mwenyekiti Yusuf Manji.Hayo yamefikiwa kwa kauli moja baada ya viongozi wa matawi kukutana na kujadiliana baada ya Shitrikisho la Mpira wa Miguu (TFF) kutangaza mchakato wa uchaguzi wa Yanga na kutaja tarehe ya kufanyika uchaguzi huo.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mkutano wao wa ndani, Mwenyekiti wa Matawi Bakili Makele amesema kuwa wao kama Yanga hawajakataa kufanya uchaguzi ila hawakubaliani na maamuzi ya TFF ya kusimamia mchakato mzima.Makele amesema kwa pamoja wameazimia kutokubali kusimamiwa mchakato wa uchaguzi na TFF kwa kuwa akidi ya kamati ya uchaguzi wa Yanga imetimia na TFF hawajafuata maagizo ya Baraza la Michezo (BMT) la kukutana pamoja ili kujadili uchaguzi huo.

"sisi kama Yanga hatujakataa kufanya uchaguzi ila BMT walitoa maelekezo kwa TFF kuwa wakae pamoja na sisi ili kuanz amchakato wa uchaguzi, ila tunashangaa wao wanaamua kuunda kamati yao ya Uchaguzi na kutangaza wanachama waanze kuchukua fomu kitu ambacho hatukubaliani nacho pia Yanga haiwezi kusimamiwa uchaguzi na TFF kwakuwa kamati yetu ya uchaguzi imetimia,"amesema Makele.

"Wanachama kwa pamoja tumefikia azimio la kusema kuwa nafasi ya Mwenyekiti haitajazwa kwani bado tunamtambua Yusuf Manji kama Mwenyekiti wetu na mkutano mkuu wa Yanga ndio wenye maamuzi ya kila kitu na wote tulikubaliana kuwa bado ni mwenyekiti wetu na nafasi zitakazojazwa ni tano tu moja ya makamu mwenyekiti na wajumbe wanne waliojiuzulu wote,"


Mbali na hilo, Mwenyekiti huyo wa matawi ameitwa na kamati ya maadili ya TFF kwenda kujieleza baada ya kutumiwa barua leo mchana ya kutakiwa kwenda na mashahidi wake akituhumiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo kukataa kufanyika kwa uchaguzi huo, kufanya mkutano wa hadhara kinyume na utaratibu.

Makele ameeleza kuwa, yeye kesho ataenda kusikiliza aliloitiwa katika kamati ya maadili ila anachokifahamu hajavunja sheria yoyote kwani Mkutano aliofanya ulikuwa ni wa viongozi wa matawi ikiwa ni kujadiliana mambo mbalimbali ya kimaendeleo.Baadhi ya wanachama wa Yanga wameonekana kukerwa na maamuzi ya TFF ya kutaka kusimamia uchaguzi wao na kusema kuwa hawako tayari kuona suala hilo linafanyika na kwa upande wao hawajakataa uchaguzi ila hawatataka wasimamiwe na TFF kwani kamati yao ya Uchaguzi ipo na inafanya kazi kutokana na kutimia kwa akidi ya wajumbe.

Kwa pamoja wameungana na mwenyekiti wao kuitikia wito la kuitwa kwake TFF na kumpa moyo kuwa hili nalo litapita na wataungana nae kuelekea huko ili kutoa ushahidi wao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...