THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Wananchi wazuia msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa wakidai shule

Wananchi wa kitongoji cha Senje, kijiji cha Samazi Wilayani Kalambo wamefanikiwa kuuzui msafara wa mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo na kumuomba kuwawezesha wapate ushirikiano wa kujenga shule ili watoto wao waweze kusoma.

Wananchi hao wameeleza kuwa shule ya msingi iliyopo karibu ni kilomita saba kutoka katika kitongoji hicho ambapo shule hiyo ipo katika kijiji cha Samazi huku watoto hao wengi wadogo wakishindwa kufika katika shule hiyo kutokana na umbali.

Kitongoji hicho cha Senje ambacho ni kipya kimeanza kukaliwa na wananchi na kuonesha maendeleo baada ya kuanza kujenga vyumba viwili vya madarasa, kuchimba shimo la choo pamoja na kuwa na mabati kwaajili ya kuezeka majengo hayo huku wakiwa na suluhisho la dharura kwa kumlipa posho mwanafunzi aliyemaliza kidato cha nne ili aweze kuwafundisha watoto wao.

Kwa upande wake Mh. Wangabo alisema kuwa shule hiyo inayojengwa katika kitongoji hicho itaanza kuwa shule shikizi ya shule ya msingi samazi hivyo watoto hao wataanza kusoma shule ya awali, darasa la kwanza hadi la tatu kasha watahamia katika shule ya msingi samazi wakati taratibu nyingine zikiendelea.

Aliongeza kuwa ili vyuma hivyo vianze kutumika ni muhimu kuwa na ofisi ya mwalimu na nyumba ya mwalimu ili halmashauri iweze kuunga mkono kwa kumleta mwaalimu na watoto waanze kusoma na kuwashauri kuongeza kasi ya ujenzi wa majengo hayo ili waweze kupewa mwaalimu haraka iwezekanvyo kwakuwa serikali ya wamu ya tano isingependa kuwaona watoto hawaendi shule.

“Kata pamoja na kijiji watasimamia hii, mkurugenzi utafuatilia kuhakikisha kwamba mtendaji wa kijiji na kata watasimamia ujenzi ule unaoendelea pale, lazima nyumba ya mwalimu isimame na ofisi ya mwali isimame na wakati huo muendelee kujipanga kuna swala la madawati watoto wasije wakakaa chini, vyoo ni uhimu ili wanafunzi watumie vyoo sio kwenda kwenye vichaka, shule haiwezi kuanza bila ya vyoo, tutaneza milipuko,” Alisisitiza.

Katika kuhakikisha jambo hilo linafanikiwa Mkuu wa mkoa alimuagiza mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya kalambo kuhakikisha wanaunga mkono kwa kununua mbao za kupaulia huku ofisi yake ikichangia bati za ofisi ya mwalimu pindi itakapokamilika.

Katika msafara huo ambao aliwepo mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mh. Julieth Binyura nae aliwataka kuhakikisha ujenzi wa shule hiyo hauishii kwenye madarasa mawili tu na hatimae kuiachia serikali mzigo wa kuendelea kujenga shule hiyo wakati kitongoji hicho hakikuwahi kuwepo.

“Serikali sasa hivi ina utaratibu wa kusajili, kama hujatimiza vigezo huwezi kusajiliwa shule, hata mkiwa mmejenga vyumba viwili lazima mujenge ili mtoto akimaliza la kwanza, la pili, la tatu anaendelea, lakini wengine wakijenga vyumab wanaishia viwili tu halafu watoto wanaanza kusomea chini ya miti hatutaki,” Alibainisha.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akiongea na wananchi wa kitongoji cha Senje, Kijiji cha Samazi, Wilayani kalambo mara baada ya msafara wake kuzuiwa na wananchi hao wakidai kujengewa shule. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akimkabdhi fedha mwalimu wa kujitolea katika kitongoji cha Senje, Kijiji cha Samazi anaewafundisha watoto wa kitongoji hicho ambao wapo mbali na shule ya msingi jambo lililowapelekea wazazi wa watoto wa kitongoji hicho kumlipa mwanafunzi huyo aliyemaliza kidato cha nne kuwafundisha watoto.