Wataalam wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Lindi SOKOINE wanaendelea kunufaika na utaalam wa Madaktari Bingwa pamoja na wataalam wengine wa afya kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili huku wakiwashukuru kwa utaalam wao.
Watalaam hao kutoka Muhimbili wanawafundisha kwa vitendo jinsi ya kutoa huduma mbalimbali kwa usahihi na kwa ubora.
Maeneo ambayo wataalam wa hospitali ya Sokoine wananufaika ni upasuaji, magonjwa ya kike na uzazi, meno, macho, watoto, magonjwa ya mfumo wa mkojo, magonjwa ya koo, pua na masikio, maabara, magonjwa ya ndani, magonjwa ya dharura pamoja na Radiolojia.
Daktari Bingwa wa upasuaji wa mfumo wa chakula na ini Godfrey Mchele amesema pamoja na kuwajengea uwezo wa kutoa huduma mbalimbali ikiwemo upasuaji pia wanaangalia changamoto zinazowakabili na kuwashauri kitaalam.
Naye Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Sokoine Dkt. Jumanne Shija ameahidi kufanyia kazi ushauri na mapendekezo yanayotolewa na watalaam hao ambao wamebobea katika kutoa huduma za afya ili wajifunze na kuleta mabadiliko katika hospitali hiyo.
‘’Tuna shukuru uwepo wenu, tuna ahidi kufanyia kazi yale yote ambayo tunashauriwa na watalaam kutoka Muhimbili ili kusudi hospitali yetu ipige hatua katika kutoa huduma bora za afya kwa wananchi’. Amesema Kaimu Mganga Mfawidhi.
Watalaam wa afya kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili wakiwemo Madaktari Bingwa 11 bado wapo katika hospitali ya Sokoine kwa ajili ya kutoa huduma za afya na kuwajengea uwezo wataalam wa hospitali hiyo.
 Daktari Bingwa wa upasuaji wa mfumo wa chakula na ini wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Godfrey Mchele (kushoto) akiwafundisha Madaktari wa Kitengo cha Upasuaji cha Hospitali ya Rufaa mkoa wa Lindi SOKOINE jinsi ya kuunganisha utumbo baada ya kukatwa.
 Daktari Bingwa wa magonjwa ya kinywa na meno kutoka Muhimbili Kessy Frank (kulia) akimuelekeza Tabibu wa magonjwa ya kinywa na meno wa hospitali ya Sokoine Benard Mpepo namna ya kutoa dawa ya ganzi kwa usahihi kabla ya matibabu ya kinywa.
 Daktari Bingwa wa upasuaji wa mfumo wa mkojo kutoka Muhimbili Edward Ogola akishirikiana na watalaam wa afya wa hospitali ya Sokoine kufanya upasuaji wa tezi dume.
 Mtaalam wa macho kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili Elizabeth Mahende akimpima mgonjwa wa macho Bwan. Karim Wahedi ili kupata namba sahihi ya miwani itakayomsaidia kuona wakati wa kusoma na wakati anapotembea.

Wananchi wa mkoa wa Lindi wakisubiri kupatiwa huduma za afya na wataalam kutoka MNH kwa kushirikiana na wataalam wa hospitali ya Sokoine hii leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...