Hyasinta Kissima
Halmashauri ya Mji Njombe imekusudia kutatua changamoto ya upungufu wa vitendea kazi kwa watendaji wa Kata katika Halmashauri hiyo kwa kuwakopesha pikipiki.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya pikipiki hizo kwa watendaji wa Kata za Lugenge, Matola, Ihanga na Kifanya  Mkuu wa Idara ya Utumishi na Utawala Halmashauri ya Mji Njombe Abdulatif Mkata amesema kuwa lengo la Halmashauri kuwakopesha pikipiki hizo ni kutoa motisha kwa watendaji waliofanya vizuri katika utendaji wao wa kazi na kurahisisha utendaji kazi wa watendaji hao wa Kata kwa kuwa Kata wanazozisimamia ni kubwa na pikipiki hizo zitawawezesha kutekeleza majukumu yao kwa urahisi kwa kuweza kufika kwenye Vijiji vya Kata na kufanikisha utoaji wa huduma kwa jamii kwa wakati.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Edwin Mwanzinga amewataka watendaji hao kuhakikisha kuwa wanazitunza pikipiki hizo na kuhakikisha kuwa zinatumika kwa ajili ya ufuatiliaji wa mapato ya Halmashauri na usimamizi wa shughuli za maendeleo katika Kata zao.
“Kwanza natoa pongezi kwa kazi nzuri mlizofanya katika Kata zenu.  Pikipiki hizi tumewapatia kama mkopo ili muweze kuzitunza kwani utakapo maliza mkopo wewe ndio utakua mmiliki halali wa pikipiki hizi. Ni matumaini yangu kuwa sasa mtaenda kusimamia shughuli za maendeleo ya Kata kwa urahisi lakini kubwa zaidi kusimamia mapato ya Halmashauri kikamilifu.”Alisema Mwanzinga.
Khadija Lutumo ni Mtendaji wa Kata ya Lugenge Halmashauri ya Mji Njombe ambaye ni miongoni mwa watendaji waliokabidhiwa pikipiki hizo ambapo ameishukuru Halmashauri kwa kutoa motisha ya pikipiki  kwani itasaidia kutatua changamoto ya uhaba wa vitendea kazi  na ameahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii katika Kata yake na kusimamia mapato kikamilifu kwani kwa kutumia pikipiki aliyokabidhiwa swala la usimamamizi litakuwa rahisi.
Halmashauri ya Mji Njombe imefanikiwa kununua pikipiki nne zenye thamani ya Shilingi milioni tisa laki 4 kupitia mapato ya ndani na imekusudia kuhakikisha kuwa katika siku za mbeleni watendaji wote watakaofanya vizuri katika maswala ya utendaji kazi na ukusanyaji mapato wanakopeshwa pikipiki  kwa kutenga  bajeti  na kuhakikisha Mazingira ya kazi ya watumishi wake yanaboreka siku hadi siku.
Ikumbukwe kuwa Halmashauri ya Mji Njombe ni miongoni mwa Halmashauri za Miji zinazofanya vizuri katika swala la ukusanyaji mapato na imejizatiti kuhakikisha kuwa kadri siku zinavyosonga mbele ikusanye zaidi ya malengo yaliyokusudiwa na kuibuka kinara  katika makusanyo ya mapato.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Edwin Mwanzinga akimkabidhi funguo ya  pikipiki Mtendaji wa Kata ya Lugenge  Khadija Lutumo wakati wa utoaji wa mkopo wa pikipiki kwa watendaji wa Kata Halmashauri ya Mji Njombe 
 Mkuu wa idara ya Utumishi na Utawala Halmashauri ya Mji Njombe Abdulatif Mkata akizungumza jambo wakati wa makabidhiano ya pikipiki hizo.Kushoto kwake ni watendaji wa Kata katika Halmashauri ya Mji Njombe
Wajumbe wa Kamati ya fedha na wataalamu wa Halmashauri ya Mji Njombe wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya makabidhiano ya pikipiki hizo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...