VICTOR MASANGU, KISARAWE

WAZIRI wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo amekemea vitendo vya upokeaji wa rushwa vinavyofanywa na baadhi ya wauguzi,wataalamu wa afya na madaktari kuwataka kuachana na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wahakikishe wanatoa huduma ya matibabu kwa wagonjwa kwa kuzingatia misingi ya weledi ya kazi yao bila kuwa na ubaguzi wowote.

Jafo alitoa kaul hiyo wakati akizungumza na wataalamu wa afya, pamoja na wananchi wakati wa sherehe za kukabidhi mashine maalumu kwa ajili ya uchunguzi wa magonjwa ya aina mbali mbali katika hospitali ya Wilaya ya Kisarawe ambapo viongozi wa serikali madiwani pamoja na viongozi wa dini waliweza kushiriki katika zoezi hilo.

Aidha Waziri Jafo alibainisha kwamba lengo kubwa la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inaboresha sekta ya afya kuanzia ngazi za maeneo ya vijijini kwa kuongeza ujenzi mpya wa zahanati, vituo vya afya pamoja na hospitali lengo ikiwa ni kuwaondolea adha wananchi katika suala zima la upatikanaji wa huduma ya matibabu kwa urahisi zaidi.

“Napenda kuchukua fura hii kuwambia ndugu zangu wananchi wa Kisarawe kwa kweli Rais wetu anafanya kazi kubwa sana ya kuhakikisha analeta maendeleo katika sekta mbali mbali hapa nchini na kwa sisi watu wa kisarawe tumepata bahati kubwa sana, kwa hiyo nipende kuwaambia tutaendelea kuboresha huduma ya afya katika zahanati zetu, vituo vya afya pamoja na ujenzi wa Hospitali nyingine mpya,”alisema Jafo.

Waziri wa chi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) kulia Selemani Jafo akikata utepe wakati wa sherehe ya kukabidhi mashine kwa ajili ya kutibu magonjwa mbali mbali katika hospitali ya Kisarawe, kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo 
Mganga mkuu wa Wilaya ya Kisarawe kulia Jonathan Budenu akifafanua jambo kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa  (TAMISEMI) Seleman Jafo mara baada ya kukabidhi mashine hizo katika hospitali ya Wilaya.  
Waziri wan chi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo kulia wakiwa na baadhi ya viongozi wengine wa serikali wa kati kati ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo na kushoto kwake ni Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Kisarawe Musa Gama katika halfa hiyo ya makabishiano ya mashine za kutibu magonjwa mbali mbali. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...