WAZIRI MKUU Kassim Majaliwaamewapongeza wakazi wa kata ya Nachingwea wilayani Ruangwa kwa kujenga shule ya msingi kwenye kijiji cha Kilimahewa. “Uamuzi wa kujenga shule ya msingi ni sahihi kwa kuwa huwapunguzia watoto kutembea umbali mrefu na pia utarahisisha mazingira ya kusomea kwa watoto wetu.” 

Waziri Mkuu ametoa pongezi hizo leo (Jumanne, Novemba 20, 2018) alipotembelea eneo la ujenzi wa shule ya msingi Lugalo na kuwataka waendelee na moyo huo. Amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli inataka kila mtoto aliyefikia umri wa kwenda shule aanzishwe shule na asome. Kadhalika, Waziri Mkuu ametaka wananchi hao waweke pembeni itikadi zao za kisiasa na badala yake washirikiane kujenga miradi ya maendeleo kwenye eneo lao. 

Nae, Mtendaji wa Kijiji cha Kilimahewa, Majuto Ungulu amesema ujenzi wa shule hiyo uliibuliwa na wakazi wa kijiji hicho, ambacho hakina shule ya msingi. Majuto amesema watoto wa kijiji hicho wanalazimika kutembea umbali wa kilomita mbili hadi shule la msingi Ruangwa, hivyo ujenzi huo utawawezesha kusoma karibu. Amesema kwa sasa wameanzia na ujenzi wa vyumba vinane vya madarasa, matundu 18 ya vyoo na ofisi mbili za walimu ambapo jumla yake ni sh. milioni 399.8. 


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Ruangwa, Novemba 20, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Hashim Ngandirwa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Ruangwa, Novemba 20, 2018.

Baadhi ya wanawake waliojitokeza kushiriki katika ujenzi wa Shule ya Msingi katika kijiji cha Kilimahewa wilayani Ruangwa wakimshangilia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowasili kwenye eneo la ujenzi wa shule hiyo kukagua ujenzi na kushiriki katika ujenzi huo, Novemba 20, 2010

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Shule ya Msingi ya kwenye kijiji cha Kilimahewa unaofanywa na wananchi wa Kata ya Nachingwea wilayani Ruangwa, Novemba 20, 2018. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...