WAZIRI MKUU Kassim Majaliwaamewataka wananchi kwenye Kata ya Mnacho wilayani Ruangwa washirikiane kujenga mabweni katika shule ya sekondari Mnacho ili kuwaondolea wanafunzi adha ya kutembelea umbali mrefu kwenda shuleni hapo.

Ameyasema hayo leo (Jumatatu, Novemba 19, 2018) wakati alipotembelea shule hiyo kwa ajili ya kukagua mradi wa ujenzi wa bweni, ambalo ujenzi wake unagharimu sh. milioni 92.4 ikiwa ni mchango uliotolewa na wadau wa elimu.

“Bweni hili likikamilika litawapunguzia wanafunzi kutembea umbali mrefu kuja shuleni hususani wanaoishi vijiji vya mbali kwa sababu wataishi hapa, jambo ambalo litachangia kuongeza ufaulu wa watoto wetu.” Kadhalika, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi waishio katika Kata hiyo na za jirani washirikiane na kuanzisha mradi wa ujenzi wa mabweni mengine kwa kuwa hilo moja lililojengwa na wadau halitoshi kulingana na idadi ya wanafunzi.

Amesema yeye yuko tayari kuendelea kuwaunga mkono wananchi hao kwenye mipango yao yote ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Kata yao, lengo likiwa ni kuhakikisha mikakati ya Serikali ya kuboresha huduma za jamii inatimia. Hata hivyo, Waziri Mkuu amewataka wananchi hao washirikiane na walimu kufuatilia maendeleo ya taaluma kwa watoto wao shuleni na kujiridhisha kama wanafanya vizuri darasani na iwapo watabaini changamoto waweze kuzitatua kwa pamoja.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu ujenzi wa bweni lenye uwezo wa kulaza wanafunzi 80 kutoka kwa Mkuu wa Shule ya Mnacho wilayani Ruangwa, David Mwakalobo wakati alipokagua ujenzi wa bweni hilo Novemba 19, 2018 . Kulia kwake ni Mkuu wa wilaya ya Ruangwa, Hashim Mgandirwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa chumba cha upasuaji katika Zahanati ya Nandagala wilayani Ruangwa, Novemba 19, 2018. Kushoto ni Mganga Mfawidhi wa Zahanati hiyo, Abubakar Abbas Rugwa. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Zahanati ya Nandagala wilayani Ruangwa Novemba 19, 2018. Kushoto kwake ni Mkuu wa wilaya ya Ruangwa, Hashim Mgandirwa, kushoto ni Mganga Mkuu wa wilaya ya Ruangwa, Dkt. Mahela Njile na kushoto ni Mganga Mfawidhi wa Zahanati hiyo, Abubakar Abbas Rugwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...