Na  Agness Francis, Globu ya Jamii. 

TIMU ya Yanga imetoshana nguvu na Ndanda FC 'wanakuchele' kwa kushindwa kupata alama 1 nyumbani kwa kutoka sare ya mabao 1-1 katika mchezo uliopigwa katika dimba la Taifa Jijini Dar es Salaam.

Mtanange huo wa aina yake ulioanza majira ya saa moja usiku na kila upande wakicheza kwa kukamiana kutafuta magoli ya ushindi ambapo kwa kipindi cha kwanza dakika 15 za mapema tu Ndanda anapata goli la kuongoza kupitia kwa mchezaji wake Vitalis Mayanga alieingiza Mpira kimnyani na kutikisa nyavu za Yanga. 

Wachezaji walionekana kuinuka zaidi wakishambuliana kwa kila upande ukiitaji matokeo zaidi lakini mpira uligeuka kwa upande wa  Yanga kuwashambulia wapinzani wao na dakika ya 24 Jafari Mohamed anaindikia Yanga goli la kusawazisha kwa pasi iliyopigwa na Ibrahim Ajibu, Ambapo wachezaji wa Yanga walionekana kupata nguvu kwa kufanya mashambulizi katika lango la Ndanda ambayo hayakuleta matokeo,na mpaka wachezaji wanaenda mapumzikoni matokeo yalikuwa ni 1-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote mbili kukamiana kutafuta magoli ya kuongoza ambapo wachezaji wa yanga walionekana kupata nafasi nyingi za kupata magoli lakini hawakuweza kuzitumia.

Vile vile hata kwa upande wa Ndanda ilikuwa hivyo kwa kupoteza nafasi walizopata, mpaka mpira dakika 90 umemalizika matokeo yalibakitkuwa 1-1.

Kocha mkuu wa kikosi cha Yanga Mwinyi Zakhera amesema Kuwa mechi ilikuwa ngumu sana na wachezaji walipambana lakini walishindwa kupata magoli,ambapo amesema watayafanyia kazi makosa waliyokosea. 

"Tumecheza sana Kwa kushambulia mpira lakini hatukuweza kushinda wachezaji walijaribu kucheza mashuti ya mbali na ya karibu lakini mpira haukuweza kuingia golini"amesema Zakhera. 

Naye kocha wa Ndanda FC Malale Khamis amezungumzia Siri ya mafanikio kwa kuweza kutoa sare ya pili,ambapo ya Kwanza alitoa na Simba SC uwanja wa Nangwanda sijaona.

"Tunatambua tunacheza na timu kubwa huwa tunaiandaa zaidi,hata hivyo nawapongeza wachezaji wangu Kwa kufata maelekezo ninayowaelekeza"amesema kocha Khamis.

Yanga akishuka nafasi ya Tatu alama 26 akiwa amefikisha michezo  10,Simba akiwa juu yake  michezo 11 alama 26,huku Azamfc wakijikita kileleni mwa ligi kuu Tanzania bara  (TPL) kwa pointi 30 michezo 12.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...