Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif AliIddi alisema Zanzibar itaendelea kuwa karibu na Muungano wa Falme za Kiarabu {UAE} katika dhana nzima ya kuimarisha Sekta ya Uchumi na Ustawi wa Jamii wa Wananchi wa pande zote mbili. Alisema hatua hiyo inakuja kufuatia mafungamano makubwa yaliyopo kati ya Zanzibar na Muungano wa Mataifa hayo hasa katika Sekta ya Biashara kwa usafirishaji wa bidhaa za Matunda na Viungo.

Balozi Seif Ali Iddi alieleza hayo wakati wa mazungumzo yake na Balozi Mpya wa Muungano wa Falme za Kiarabu {UAE} Bwana Khalifa Abdulrahman Mohamed Al – Marzooqi aliyefika Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar kujitambulisha rasmi. Alisema kutokana na utulivu mkubwa uliopo Zanzibar ulioambatana na Miundombinu sahihi ya Uwekezaji Wawekezaji wa Mataifa hayo wana fursa nzuri ya kutumia nafasi hiyo ikiwa ni njia ya kuendeleza uhusiano wa muda mrefu uliopo kwa sehemu hizo mbili.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimueleza Balozi huyo wa Muungano wa Falme za Kiarabu { UAE} kwamba wakati umefika kwa watendaji wake kufuatilia kwa kina mambo yaliyokubalika katika Mikutano na Vikao kufuatia ziara ya Rais wa Zanzibar aliyoifanya katika Mataifa hayo rafiki miezi michache iliyopita.

Balozi Mpya Bwana Khalifa Abdulrahman Mohamed Al – Marzooqi wa Muungano wa Falme za Kiarabu {UAE} kati kati akisabahiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipofika Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar kujitambulisha rasmi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisisitiza umuhimu wa Wawekezaji wa Muungano wa Falme za Kiarabu kutumia fursa za Uwekezaji zilizopo Tanzania kuanzisha Miradi yao.
Balozi Khalifa Abdulrahman Mohamed Al – Marzooqi wa Muungano wa Falme za Kiarabu {UAE}akimueleza Balozi Seif shauku ya Wafanyabiashara wa Mataifa ya Muungano wa Falme za Kiarabu kutaka kuwekeza Zanzibar kutokana na mazingira mazuri ya Miradi ya Kiutalii. Picha na – OMPR – ZNZ.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...