Na Khadija Seif, Globu ya Jamii

UMOJA wa wafugaji bata nchini wamekutana na kuzindua tamasha la uchomaji wa  nyama ya Bata  katika ukumbi wa police officers mess jijini Dar es salaam.

Akifungua hafla hiyo ya tamasha la uchomaji nyama ya bata Afisa mifugo wa jamii ya ndege Deodratus Nestory kutoka Manispaa ya Kinondoni  
 amewapongeza  wafugaji hao na kusema kuwa ni   nadra sana kukuta tamasha la uchomaji nyama ya bata kwani imeshazoeleka mbuzi choma na kuku choma.

Nestory amesema kuwa "Umoja huu upo kwa ajili ya  kutia watu hamasa ili waweze kutambua thamani ya nyama ya bata, na Manispaa ya Kinondoni itatoa semina kwa wafugaji wote wa mbuzi,ngombe, kuku na bata ili waweze kupata masoko kwa urahisi na  kuwapa ushirikiano kutoka Serikalini kuanzia Manispaa hadi Wizara husika ya Kilimo na ufugaji" amesema Nestory.

Pia Nestory amefafanua kuwa kufikia mwakani  watafungua chama cha wafugaji wa jamii ya ndege ambacho kitatambulika kisheria
Ili waweze kupata mkopo kutoka mabenki tofauti na kuwawezesha kupanua soko na ufugaji wenye tija.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyowakutanisha wafugaji wa Bata kutoka sehemu mbalimbali yakiwemo Kawe, Kibiti,Morogoro,kigamboni na Bunju  Mwenyekiti wa chama hicho Riziki osward amesema sasa ni wakati wa kumpa thamani bata pamoja na nyama ya bata kwani jamii bado haina mwamko katika Kula kwa wingi nyama hiyo.

Hata hivyo osward amefafanua zaidi kuwa lengo la tamasha hilo sio tu Kula nyama peke yake bali hata kujifunza  namna bora ya kufuga bata hao hasa katika kuanzia malisho ,madawa na chakula.

Pia ameeleza kuwa mikakati ya Umoja wa wafugaji bata itahakikisha inatoa elimu kwa wafugaji na kuwasaidia ili kuweza kupanua soko na kumpa thamani bata kwani bado kuna desturi iliyojengeka juu ya bata kuwa ni mchafu japo bata ana thamani kubwa kuliko kuku .

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...