Benki ya NMB imetoa msaada wa Stuli 32 na meza 8 za maabara zenye thamani ya Shilingi milioni tano ili kusaidia wanafunzi kujifunza kwa vitendo masomo ya sayansi katika shule ya Sekondari Mwantini iliyopo katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga. 
 

Msaada huo umekabidhiwa leo Alhamis Desemba 6,2018 na Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi James Katamba kwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga,Mheshimiwa Jasinta Mboneko.

Katamba alisema msaada huo wa stuli na meza ni sehemu ya ushiriki wa benki hiyo katika maendeleo ya jamii akibainisha kuwa changamoto za sekta ya elimu nchini kwa NMB ni jambo la kipaumbele kutokana na kwamba elimu ni uti wa mgongo wa taifa lolote duniani. “NMB tulipokea maombi kuwa mnahitaji stuli na meza za maabara,tulifarijika na kuamua kuja mara moja kushirikiana nanyi ili kuwa chachu ya maendeleo ya elimu kwa watoto wetu katika shule hii”,alieleza.

“Tunatambua kuwa kupitia jamii ndipo wateja wetu wengi wanapotoka,kwa hiyo kurudisha sehemu ya faida kwa jamii ni utamaduni,tutaendelea kuunga mkono juhudi za wadau wetu kuhakikisha changamoto za jamii zinapatiwa ufumbuzi”,aliongeza Katamba. Hata hivyo alisema kwa mwaka 2018,NMB imetenga zaidi ya shilingi bilioni 1  kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya wananchi ikiwemo kusaidia sekta ya afya na elimu hivyo kuifanya benki ya NMB kuwa benki ya kwanza kuchangia maendeleo kuliko benki yoyote nchini.

Kulia ni Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi James Katamba akishikana mkono na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mheshimiwa Jasinta Mboneko wakati wa zoezi la kukabidhi stuli 32 na meza 8 za maabara kwa ajili ya shule ya sekondari Mwantini.Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa  ALAT taifa,mheshimiwa Gulam Hafeez Mukadam ambaye pia ni Mstahiki meya wa Manispaa ya Shinyanga.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mheshimiwa Jasinta Mboneko na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Ngassa Mboje wakipokea moja kati ya stuli 32 kutoka benki ya NMB. Kulia ni Meneja wa Benki ya NMB Manonga,Baraka Ladislaus na Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi James Katamba.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mheshimiwa Jasinta Mboneko akisalimiana na wanafunzi wa shule ya sekondari Mwantini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...