Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu imesema kuwa haiwezi kuwavumilia wananchi wanaharibu vyanzo vya maji.  Hayo ameyasema Afisa   wa Maji Bonde la Wami/Ruvu Simon Ngonyani wakati akizungumza na waandishi habari kuhusiana na wananchi kufanya shughuli mbalimbali ndani ya mita 60 katika vya vyanzo vya maji ambapo wameweza kukata mazao mbalimbali katika eneo la Ruvu.

Amesema Bonde la Wami/Ruvu  ilishatoa elimu kwa wananchi kuacha kufanya shughuli za kilimo ndani ya mita 60 lakini utekelezaji wake umekuwa wa ukisuasua na kulazimika kuvyeka mazao  yaliyokuwa yanalimwa na wananchi hao.

Simon amesema kuwa vyanzo vya maji lazima vilindwe kwani wananchi wakikosa huduma za maji watawalalamikia  serikali hasa wale watu waliopewa dhamana ya kusimamia.  Aidha amesema wananchi wa Ruvu kila walipokutana walikuwa wanasema wakishavuna wanaacha kilimo hicho katika Kingo mto Ruvu matokeo yake walikuwa wakivuna na kupanda tena na kuomba tena ambapo ukawa ndio mchezo wao.

Hata hivyo amesema kuwa wananchi waliopo katika Bwawa la Mindu Morogoro walishalipwa tangu mwaka 1970 matokeo yake watu wanauziana maeneo hayo wakitaka kuwaondoa wanadai fidia wakati watu walishalipwa. Amesema hatabaki  mtu salama kwa kutokana na vitu vyote viko kisheria katika kulinda vyanzo vya maji na wasimamizi wako.
Ngonyani amesema kuwa watu wafuate sheria kwani wakiwa kinyume na sheria watakuwa wanalalamika tu huku wakijua walikuwa wamevunja sheria. "Mimi nitaendelea kusimamia sheria na ndio kazi yangu ili kuhakikisha vyanzo vya maji vinatumiwa kwa uangalifu"amesema Ngonyani.
Afisa wa Maji Bonde la Wami/Ruvu Simon Ngonyani akizungumza na waandishi habari kuhusiana na hatua wanazozichukua katika utunzaji wa vyanzo vya maji katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...