Na Heri Shaban

MKUU wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema jijini Dar es Salaam ameanza kukabidhi vitambulisho vya wafanyabiashara wadogowadogo maarufu kama Wamachinga waliopo Kariakoo.

Mjema amegawa vitambulisho hivyo Dar es Salam ikiwa ni siku mbili tu zimepita baada agizo la Rais John Magufuli kuwagiza wafanyabiashara wote watambulike wakiwa na vitambulisho hivyo vinavyotolewa vya Wajasiriamali wadogo.

"Katika Wilaya yangu ya Ilala leo(jana) nimegawa vitambulisho 5000 kwa Wamachinga wa Kariakoo ambao tulikuwa tunawatambua katika mfumo maalum, zoezi hili baadae litahamia kwa Mama lishe wote waliopo wilayani Ilala ambao mtaji wao chini ya shilingi milioni nne," alisema Mjema

Amesema katika wilaya ya Ilala mchakato huo umekwenda vizuri kwani wamachinga walishawekwa pamoja katika mfumo maalum ambao wanatambulika rasmi na Serikali. Aliwataka Wamachinga na wafanyabiashara wote kufuata utaratibu na wote watapewa vitambulisho hivyo katika ofisi za Halmashauri zilizopo jengo la Anatogluo.

Aidha amesema wote waliopewa vitambulisho wanatambulika na biashara zao na maeneo kama sio mfanyabishara hawezi kupewa.Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Elzabeth Thomas amesema Manispaa ya Ilala wamejipanga vizuri katika juhudi za kumsaidia Rais na tayari wameanza na Wamachinga wa Kariakoo wote.

Thomas amesema mpango huo wa kugawa vitambulisho ni endelevu mpaka wote wapewe vitamburisho Watendaji wake wa Manispaa hiyo wanasimamia. Naye Makamu Mwenyekiti wa Wamachinga Kariakoo Yusuph Namoto amesema wao ni wazalendo wanaungana na Serikali yao tukufu katika juhudi za kumsaidia Rais katika kukuza uchumi.Yusuph amesema kwa sasa wanahitaji kukuza uchumi biashara zao kila wakati zinabadilika hivyo wanaitaji uwezeshaji ili waweze kupiga hatua. 
Mkuu wa wilaya ya Ilala sophia Mjema akimkabidhi kitambulisho mfanyabiashara mmachinga Ramadhan Said Dar es Salam jana ,wengine OFISA Masoko Ilala na Ofisa Biashara wa Manispaa wakishudia tukio hilo.Picha na Heri Shaaban.
 Makamu Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wamachinga Yusuph Namoto akionyesha KITAMBURISHO chake mara baada kukabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema Dar es Salam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...