Na Is-Haka Omar, Zanzibar
WATENDAJI wa Serikali za Mitaa nchini wametakiwa kujenga utamaduni wa kufanya ziara za kiutendaji kwa wananchi wa ngazi zote ili kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu changamoto zinazowakabili wananchi. Rai hiyo ameitoa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla Mabodi katika mwendelezo wa ziara zake za kukagua utekelezaji wa Ilani katika Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini 'A' Unguja.

Amesema lazima watendaji na viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia mfumo wa ugatuzi washuke kwa wananchi kwa lengo la kufuatilia masuala mbali mbali yatakayosaidia kumaliza changamoto zinazowakabili wananchi katika ngazi za serikali za mitaa. "Lengo la Serikali Kuu kushusha madaraka katika Serikali za Mitaa kupitia dhana ya ugatuzi ni kuongeza ufasini wa uimarishaji wa huduma za kijamii kwa wananchi, hivyo watendaji nyote mlioaminiwa na kupewa dhamana ya kuwahudumia wananchi lazima muwe katibu na jamii", amesisitiza Dk.Mabodi.

Katika maelezo yake Naibu Katibu Mkuu huyo, amewataka wamewasihi watendaji hao kuwa wabunifu katika kuibua miradi mbali mbali ya kijamii inayoweza kuongeza ufanisi wa kutoa huduma bora kwa wananchi. Pia Dk. Mabodi kupitia ziara yake hiyo ameelezea kuridhishwa kwake na utendaji mzuri wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini 'A' katika kutekeleza vizuri miradi inayotekelezwa kupitia ugatuzi.
 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla Mabodi akizungumza na Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kaskazini 'A' katika mwendelezo wa ziara yake katika Mabaraza ya Manispaa na Halmashauri za Wilaya Unguja.
 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla Mabodi akionyesha moja ya ripoti za ukaguzi wa miradi ya mfuko wa maendeleo wa majimbo huku akisisitiza uwajibikaji na uwazi juu ya matumizi ya fedha zinazotolewa na Wabunge na Wawakilishi Zanzibar.
 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla Mabodi akiwa na wananchi wa shehia ya Mbuyu Tende wakielekea kukagua mradi wa umeme na maji katika kijiji cha Zingani.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla Mabodi akigagua mashine ya kukoboa mpunga aina ya G-20 inayomilikiwa na kikundi cha ushirika wa 'Nguvu kazi tusizembee' huko Shehia ya Kisongoni Wadi ya Kinyasini Unguja.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...