Serikali imeitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)  kuelekeza nguvu zaidi kuhakikisha mianya ya rushwa ndani ya taasisi za umma na jamii kwa ujumla inadhibitiwa ipasavyo ikiwa ni pamoja na kutowaonea haya wanaobainika kujihusisha na vitendo vya rushwa bila kujali vyeo vyao. Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati akifunga mkutano mkuu wa siku mbili wa mwaka wa viongozi wa TAKUKURU nchini uliofanyika katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa, jijini Dodoma.
Mhe. Mwanjelwa amesema, watumishi wote wa TAKUKURU wamekula kiapo na wamepewa dhamana ya kuzuia na kupambana na rushwa, hivyo wametakiwa kutomuogopa mtu yeyote anayejihusisha na rushwa na kumshughulikia ipasavyo kwa mujibu wa sheria.
Mhe. Mwanjelwa ameongeza kuwa, katika kutekeleza azma ya serikali kufikia uchumi wa kati wa viwanda, TAKUKURU ikiwa ni taasisi iliyopewa dhamana na serikali ya kupambana na rushwa, haina budi kudhibiti vitendo vya rushwa katika sekta zilizopewa kipaumbele katika Mkakati wa Kitaifa Dhidi ya Rushwa na Mpango wa Utekelezaji Awamu ya Tatu (NACSAP III).
Mhe. Mwanjelwa ameziainisha sekta zilizopewa kipaumbele, kuwa ni pamoja na sekta ya manunuzi ya umma, ukusanyaji wa mapato, maliasili na utalii, madini, gesi, afya, elimu na ardhi, hivyo TAKUKURU kuanzia ngazi ya wilaya inapaswa kutoa mchango kufikia uchumi wa kati wa viwanda. Aidha, Mhe. Mwanjelwa amerejea maelekezo ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) kwa TAKUKURU alipokuwa akifungua mkutano huo ya kuwataka wadhibiti mianya ya rushwa katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwakani ambapo nae amesisitiza vitendo vya rushwa vidhibitiwe kikamilifu kwani ni kikwazo cha upatikanaji wa viongozi wenye sifa na uadilifu.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na viongozi wa TAKUKURU nchini wakati akifunga mkutano mkuu wa mwaka wa siku mbili wa viongozi hao uliofanyika katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa, jijini Dodoma.
Viongozi wa TAKUKURU nchini wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati akifunga mkutano mkuu wa mwaka wa siku mbili wa viongozi hao uliofanyika katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa, jijini Dodoma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...