Na Greyson Mwase, Mtwara 

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amezitaka halmashauri zote nchini kutokutoza kodi zilizofutwa kwenye madini ya chumvi ili wazalishaji wa madini hayo waweze kufanya kazi katika mazingira mazuri na kulipa kodi stahiki serikalini. 

Naibu Waziri Nyongo ameyasema hayo leo Desemba 12, 2018 kwenye mkutano wake na wazalishaji wa madini ya chumvi kutoka katika Chama cha Wazalishaji wa Madini katika Mkoa wa Mtwara (MTWAREMA) kilichofanyika kwenye Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mtwara mjini Mtwara ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku mbili katika mkoa huo yenye lengo la kukagua shughuli za uchimbaji wa madini pamoja na kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wa madini. 

Alisema kuwa, Serikali ya Awamu ya Tano kupitia Wizara ya Madini iliamua kufuta baadhi ya kodi walizokuwa wanatozwa wazalishaji wa madini ya chumvi ambazo zilikuwa ni mzigo kwao na kushindwa kufikia malengo waliyojiwekea. “Ninaziagiza halmashauri zote nchini kutoza kodi kwa kuzingatia sheria zilizopo huku zikihakikisha kodi zilizofutwa kisheria hazitozwi tena.” Alisema Naibu Waziri Nyongo. 

Akielezea mikakati ya Serikali kupitia Wizara ya Madini katika kuwasaidia wazalishaji wa madini ya chumvi katika mkoa wa Mtwara, Naibu Waziri Nyongo alieleza kuwa ni pamoja na kuangalia namna ya uanzishwaji wa kiwanda cha chumvi katika mkoa wa Mtwara kwa ajili ya kuongeza ubora na thamani ya madini ya chumvi. 
Kutoka kushoto, Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo, Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mtwara, Mhandisi Ephraim Mushi, Msaidizi wa Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo, Mhandisi Noel Baraka wakipata  maelezo kutoka kwa Mhandisi Migodi Mwandamizi kutoka Ofisi ya Madini ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mtwara, Mhandisi Aidan Mhando kwenye eneo la uchimbaji wa mchanga la Ziwani lililopo Wilayani Mtwara mkoani Mtwara. 
Afisa Tarafa wa Ziwani, Fransis Mkuti (kushoto) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kulia) kwenye eneo la uchimbaji wa mchanga la Ziwani lililopo Wilayani Mtwara mkoani Mtwara.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati) akichimba mchanga pamoja na wachimbaji wa madini ya mchanga kwenye eneo la uchimbaji wa mchanga la Ziwani lililopo Wilayani Mtwara mkoani Mtwara. 
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akikagua madini ya chumvi katika ghala la kuhifadhi madini hayo kwenye shamba la chumvi linalomilikiwa na Jeshi la Magereza la Kiwanda Chumvi lililopo wilayani Mtwara mkoani Mtwara. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...