Na Editha Shija, Tabora

HALMASHAURI ya Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wilayani humo wamejipanga kumaliza kero ya maji kwa wananchi ambayo imekuwa ya muda mrefu katika maeneo karibu yote wilayani humo.

Akizungumza na Michuzi Blog ofisini kwake jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Dk.John Pima alibainisha kuwa ushirikiano mzuri wa watendaji na wataalamu wa halmashauri umechochea kasi nzuri ya ukusanyaji mapato, hivyo kumewezesha miradi mingi ya maji kutekelezwa kwa asilimia 100.

Amesema kuwa mfuko wa programu ya maji umekuwa chachu ya kufanikisha utekelezaji wa miradi hiyo na wana uhakika katika kipindi kifupi kijacho tatizo la maji litapungua kwa kiasi kikubwa kama si kumalizka kabisa.Pima ameongeza kutafuta ufumbuzi wa changamoto ya upatikanaji maji , ametaja miradi ya maji iliyotekelezwa kwa asilimia zote ni ujenzi wa mantenki mawili ya kuvunia maji mvua yenye ujazo wa lita 50,000 yaliyojengwa katika Shule ya Sekondari ya Uyowa na Mkindo na ujenzi wa tenki La chini ya ardhi lenye ujazo wa Lita 10,0000 lililojengwa katika Shule ya Sekondari ya Kaliua.

Miradi mingine iliyokamilishwa ni ukarabati wa visima virefu 4 katika vijiji vya uhindi viwili Songambele(1) Mwendakulima (1) pamoja na tenki moja la kuvunia maji ya mvua lenye ujazo wa Lita 50,000 katika zahanati ya kangemeAliongezea kwa kusema kuwa mradi mingine ni wa tenki la chini lenye ujazo wa Lita 10,0000 uliojengwa na kampuni ya FUM katika zahanati ya Nyasa huku kampuni ya wachina ya CHICCO iliyokuwa ikitengeneza barabara ya kaliuwa -Kazilambwa ikiwajengea miradi mitano ya maji.

Hata hivyo mkurugenzi huyo amewataka wananchi watunze miradi hiyo ili idumu kwa muda mrefu na kuwaondolea kero ya maji ya muda iliyokuwa inawakabiri.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...