Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Florens Luoga amesema hawaoni sababu ya kubalisha sarafu na kwamba zilizopo zinatosha na wanataka ziwe nyingi zaidi kwa lengo la kuhakikisha noti zilizopo zinatumika kwa muda mrefu.

Profesa Florens ametoa kauli hiyo leo Mjini Dodoma wakati anajibu baadhi ya maswali ya waandishi wa habari za fedha na uchumi kabla ya kufunga semina ya mafunzo ya uandishi wa habari zinazohusu fedha na uchumi iliyoandaliwa na BoT.

Ambapo waandishi walitaka kufahamu kama Tanzania nayo itabadili sarafu yake kama ambavyo nchi ya Kenye imefanya kwa kutoa sarafu mpya ambapo amesema hakuna mpango huo kwa sasa."Tanzania tuna sarafu za kutosha na tunataka ziwe nyingi zaidi ili zitumike kwa wingi na lengo ni kuona noti zetu zinaishi muda mrefu zaidi.Kuhusu Kenya na uamuzi wa kubadili sarafu yao ni uamuzi wao na hauna tatizo kwenye uchumi wetu," amesema.

Hata hivyo amesema wakati Kenya imeamua kufanya uamuzi wa kutoa sarafu mpya tayari Jumuiya ya Afrika Mashariki imeshapitisha sheria ya Benki ya Afrika Mashariki na ifikapo mwaka 2024 nchi wanachama zinatakiwa kuwa na sarafu moja.Pia ametumia nafasi hiyo kuzungumzia ubora wa noti ya Tanzania ambayo asilimia 100 inatengenezwa kwa pamba , hivyo kuifanya kuwa imara zaidi kuliko Dola."Noti yetu ni imara sana na ukiwambia watu uimara wake ni zaidi ya Dola wanaweza wasiamini."
 Gavana wa  Benki Kuu Profesa Florens Luoga akifafanua jambo wakati anazungumza na waandishi wa habari za fedha na uchumi ambapo ametumia nafasi hiyo kuzungumzia sarafu ya Tanzania
 Mkurugenzi wa BoT tawi la Dodoma Richard Wambali akitoa neno la shukrani kwa Gavana wa BoT Profesa Florens  Luoga kabla ya kufunga mafunzo ya habari za fedha na uchumi kwa waandishi wa habari
Meneja wa Idara ya Uhusiano kwa umma na Itifaki kutoka BoT Zaria Mbeo akitoa majumuisho ya mafunzo ya habari za fedha na uchumi kwa Gavana BoT Profesa Florens Luoga

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...