NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
KAMATI Maalumu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar imekutana chini ya Mwenyekiti wake ambaye pia ni Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein, imeunga mkono juhudi za Serikali kusaini Makubaliano ya Mgawanyo wa Uzalishaji wa Mafuta na Gesi Asilia (PSA) na Kampuni ya RAKGAS ya Ras al Khaimah ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Akitoa ufafanuzi jana Disemba 11, mwaka 2018 juu ya masuala mbali mbali yaliyoazimiwa kupitia Kikao hicho Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar  Dk.Abdulla Juma Saadalla 'Mabodi', huko Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui, ameeleza kwamba Kikao hicho kimeipongeza Serikali kwa kusaini mkataba huo na kueleza kuwa ulifuata taratibu zote za kisheria.

Dk. Mabodi aliongeza kwamba maamuzi ya kusaini mkataba huo yametokana na kukamilika kwa taratibu mbali mbali za kisheria kwa pande zote za Muungano ambapo kupitia maamuzi ya kisheria Zanzibar imepewa mamlaka ya kuchimba na kusimamia yenyewe masuala ya Mafuta na Gesi.

Alisema kuwa kufanikiwa kwa mchakato huo wa kusainiwa mkataba huo ni hatua kubwa ya maendeleo iliyofanywa na Dk.Ali Mohamed Shein, kwa kushirikiana na Viongozi mbali mbali wakiwemo Rais Mstaafu wa awamu ya nne  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jonh Pombe Magufuli.
WAJUMBE wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar wakiwa katika Kikao cha kawaida kinachofanyika mara moja kila baada ya miezi mitatu, huko Kisiwandui Afisi Kuu Zanzibar.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...