Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa ametaka kero ya maji kwa wakazi wa Mtoni itatuliwe haraka iwezekanavyo mara baada kujionea hali huduma ya maji kwa wananchi. 

Amezungumza hayo katika muendelezo wa ziara yake ya kusiskiliza kero za wananchi jijini Dar es Salaam, na kuitaka DAWASA itafute suluhisho la kufikisha huduma ya maji kwa wananchi, ukizingatia uwepo wa chanzo cha maji na mtambo wa kusafishia maji katika eneo la Mtoni.

Profesa Mbarawa amesema haoni sababu ya wananchi hao kukosa maji kwa kuwa kuna chanzo cha maji cha uhakika, kinachohitajika ni kuweka mkakati mzuri wa ujenzi wa miundombinu itakayofikisha maji kwa wananchi kwa kuwa chanzo kipo. Akiwa kwenye Mtaa wa Mashine ya Maji, Profesa Mbarawa amekutana na kero ya maji kutoka kwa wananchi ambao wamesema maji wanayotumia yanayotoka kwenye kisima usalama wake ni mdogo, kumuomba Waziri wa Maji awatatulie changamoto hiyo.

Aidha, wamemuomba Waziri wa Maji aipatie ufumbuzi changamoto ya kisima kilichochimbwa na Halmashauri ya Temeke kilichokuwa kikitumika awali kwa ajili ya kutoa huduma ya maji kwa wananchi kuhodhiwa na mtu binafsi wakati wao wakiwa na uhitaji mkubwa wa maji. Akijibu hoja za wananchi hao Profesa Mbarawa amesema atatuma timu ya wataalamu wa DAWASA ifike eneo hilo Jumatatu ijayo, ili waweze kufuatilia jambo hilo kabla ya kuchukua hatua zinazostahili. Pia, waangalie namna jinsi watakavyoweza kufanikisha zoezi la kufikisha huduma ya maji kwa wakazi hao.

Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa amemaliza ziara yake ya siku tano katika Jiji la Dar es Salaam; ambapo ametembelea maeneo yenye changamoto kubwa ya upatikanaji wa maji ya Kimara, Bonyokwa, Salasala na Mtoni kusikiliza kero za wananchi ambazo amekuwa akizisikia kwa lengo la kuzipatia ufumbuzi. Pamoja na Kiwalani ambapo alikwenda kupata mrejesho kutoka wa wananchi kuhusu maendeleo ya Mradi wa Maji Kiwalani uliozinduliwa hivi karibuni.
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akijibu hoja za wananchi mara baada ya kusikiliza kero zao eneo la Mtoni, katika Wilaya ya Temeke. 
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akimsikiliza mmoja wa wakazi wa Mtoni, Wilaya ya Temeke wakati akielezea kero yake kuhusu maji. 


Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akimsikiliza Meneja wa Mtambo wa Maji Mtoni, Mhandisi Deusdedit Rwegasila alipokuwa ziarani katika eneo la Mtoni, wilayani Temeke. 
Fundi Sanifu Mwandamizi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Robert Chenge akitoa maelezo kuhusu hali ya huduma ya maji kwa Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa alipokuwa eneo la Mtoni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...