Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
MAONESHO ya tatu ya bidhaa za viwanda vya Tanzania na siku ya viwanda Afrika yamezinduliwa rasmi yakiwa na kauli mbiu ya  "Sasa Tunajenga Tanzania ya Viwanda" huku matumizi ya teknolojia katika kutafuta masoko ndani na nje ya nchi yakisisitizwa.

Akifungua maonesho hayo Naibu waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji Mhandisi Stellah Manyanya amesema kuwa, serikali ya awamu ya tano imejizatiti katika kuhakikisha mpango kazi wa kuyafikia maendeleo unafanikiwa na kufikia 2025 wananchi wote wawe na vipato vya kati.

Aidha amesema kuwa uhakika wa masoko kwa bidhaa zinazozalishwa ni muhimu sana hasa kwa kutangaza bidhaa hizo ndani na nje kupitia maonesho ya aina hiyo.

Aidha amezipongeza taasisi 513 zilizoshiriki maonesho hayo na kuahidi kuwa Serikali kupitia Wizara ya viwanda itaendelea kuratibu na kuunganisha sekta zote katika kuhakikisha sekta hiyo inakua imara zaidi.

Pia amewataka wafanyabiashara watumie kliniki ya biashara iliyoanzishwa kwa kupeleka kero zao ili ziweze kutatuliwa na amewataka maafisa biashara ya Halmashauri na Wilaya kusikiliza kero za wafanyabiashara na kuziwakilisha mahala husika.
 Kulia  Mkurugenzi wa masoko na huduma kwa wateja wa Shirika la bima la taifa (NIC), Elisante Maleko akitoa maelezo ya bima ya kilimo kwa Naibu Waziri wa Viwanda biashara na uwekezaji,Mhandisi Stella Manyanya  ambapo akitoa wito kwa wakulima ote nchini  kujiunga na bima ya Taifa katika  maonyesho ya tatu ya bidhaa za wiwanda vya hapa nchini yaliyo funguliwa leo jijini Dar es Salaam.
  Naibu Waziri wa Viwanda biashara na uwekezaji,Mhandisi Stella Manyanya akisalimia na Mkurugenzi wa masoko na huduma kwa wateja wa Shirika la bima la taifa (NIC), Elisante Maleko leo alipotembelea banda la (NIC) katika maonyesho ya tatu ya bidhaa za wiwanda vya hapa nchini yaliyo  funguliwa leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Viwanda Biashara na uwekezaji,Mhandisi  Stella Manyanya akimsikiliza Mkurugenzi mtendaji wa wakala wa mafunzo kwa njia ya mtandao,Charles Senkondo alipotembelea banda la banda hilo katika maonesho ya tatu ya bidhaa za wiwanda vya hapa nchini yaliyo funguliwa leo jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Viwanda biashara na uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya na Mkurugenzi mtendaji wa wakala wa mafunzo kwa njia ya mtandao Charles Senkondo wakiangalia namna ya kufanya mkutano kwa njia ya mtandao leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wananchi waliofika kwenye banda la NIDA ndani ya maonyesho ya Tatu ya Bidhaa za viwanda wakipatiwa elimu juu ya zoezi la usajili, umuhimu wa Vitambulisho vya Taifa na taratibu za kufuata ili kukamilisha hatua za awali za usajili.Picha na Emmanuel Massaka wa MMG)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...