Natumia fursa hii kuwafahamisha wajumbe wote wa Baraza la Vyama vya Siasa kuwa, nimepokea taarifa rasmi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa, tarehe 20 Disemba, 2018 kutakuwa na zoezi la uteuzi wa wagombea Katika Jimbo la Temeke Dar-es Salaam na Kata 48 zilizopo katika maeneo ya Wilaya mbalimbali za Tanzania Bara.

Kimsingi, matukio yote mawili, uteuzi wa wagombea wa ubunge na udiwani uliopangwa kufanyika tarehe 20 Disemba, 2018 na kikao cha Baraza la Vyama vya Siasa kilichopangwa kufanyika tarehe 21 na 22 Disemba, 2018 ni muhimu na hayo yote yanahusisha wadau walewale. Tofauti ni kuwa, ni rahisi kuahirisha kikao cha Baraza la Vyama vya Siasa kuliko kuahirisha siku ya uteuzi wa wagombea.

Hivyo, Kwa mujibu wa Kanuni ya 16(4) ya Kanuni za Baraza la Vyama vya Siasa, nimeshauriana na wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa na tumeamua kuahirisha kikao cha Baraza la Vyama vya Siasa mpaka baada ya uchaguzi mdogo wa tarehe 19 Januari, 2018, ili kuwezesha Vyama vya Siasa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mdogo wa tarehe 19 Januari, 2018.

Tunaomba samahani kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...