*Amuuliza anataka demokrasia ya aina gani?
*Amshangaa kwa kushindwa kusema ahsante 

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

RAIS Dk.John Magufuli ameamua kujibu Mbunge wa Jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam John Mnyika baada ya kutoa malalamiko ya kudai kwamba hivi sasa demokrasia imebanwa.

Mnyika baada ya kupewa nafasi ya kusalimia wakati wa uwekwaji wa jiwe la msingi katika uzinduzi wa ujenzi wa barabara kutoka Kimara Stop over hadi Kibaha mkoani Pwani uliofanyka leo alitumia nafasi hiyo kutoa kilio chake kwa Rais Magufuli kudai demokrasia.

Hivyo Rais Magufuli pamoja na mambo mengine aliamua kumjibu Mnyika na kumuuliza anataka demokrasia ya aina gani huku akifafanua demokrasia ipo na ndio maana hata Mnyika amepata nafasi ya kuzungumza mbele yake na kwenye uzinduzi wa ujenzi wa barabara hiyo wanachama wa vyama vyote wapo na wamechanganyika bila tatizo lolote.

"Tunafahamu hata Meya wa Jiji la Dar es Salam ni wa upinzani lakini anajua kuwa Ilani inayotekelezwa ni ya CCM.Tungekuwa wabaya tusingefanya mambo ya maendeleo Dar es Salaam ambako watu walikukataa lakini bado Serikali inaleta maendeleo bila kujali.

"Mnyika kero yake kubwa ilikuwa maji kila siku lakini Serikali imetekeleza kwa kutumia mabilioni ya fedha.Nilitegemea anaposimama hapa angesema ahsante kwa Serikali kwa kutatua changamoto ya maji lakini ameshindwa na sasa anazungumzia demokrasia,"amesema.Rais Magufuli wakati anamjibu Mnyika ameendelea kueleza kuwa "Mnyika anataka demokrasia ya aina gani, amekuja hapo na kwenye mkutano ambao Mwenyekiti wake ni wa CCM, vyama vyote vipo, anataka demokrasia ya aina gani?

"Amekuja hapa amezungumza yote ambayo anayataka sasa anataka demokrasia ya aina gani.Demokrasia ndio hii amezungumza lakini 
demokrasia ya kufanya maandamano na fujo hiyo kwangu hapana.Kwanza demokrasia nzuri imehamia Dodoma.Hata kuwa bungeni na kisha kufunga mdomo nayo ni demokrasia,"amesema.

Rais Magufuli amesema Serikal anayoingoza ni kwa ajili watu na amekabidhiwa kwa ajili ya kuwatumikia WAtanzania na hivyo ataendelea kuleta maendeleo na kwamba huu ni wakati wa kuitengeneza Tanzania yetu.

"Na katika kipindi hiki hizi fedha ambazo leo zinatumika kutengeneza barabara siku za nyuma zilikuwa zinakwenda sehemu nyingine.Msiniulize ziliuwa zinakwenda wapi?Tukazibi mianya ya upotoaji wa fedha . Tulipoingia tulianza kwa kuongeza ukusanyaji kodi na tukarekebisha bajeti ambapo fedha za maendeleo ni asilimia 40 wakati zamani ilikuwa asilimia 20,"amefafanua Rais Magufuli.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kumpongeza Mbunge wa Kibamba  John Mnyika (CHADEMA) wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la Msingi la Ujenzi wa Upanuzi wa barabara ya Morogoro Kuanzia Kimara hadi Kibaha yenye Urefu wa Kilometa 19.2 .Hafla iliyofanyika Kimara Jijini Dar es Salaam Desemba 19, 2018.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...