Karama Kenyunko, Globu ya Jamii

 MAWAKILI zaidi ya 800 ambao wamehojiwa kuhusu masuala mbalimbali ya sheria wameshindwa kujieleza kwa lugha ya Kingereza kwa ufasaha. 

Imeelezwa kuwa mawakili walio wengi bado wana changamoto licha ya sheria kutumia zaidi lugha ya Kingereza.

Hayo yamesemwa leo  na Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahimu Juma ameyasema hayo leo Desemba 14, 2018 wakati wa hafla ya kuwakubali mawakili wapya 909 iliyofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Sheria kwa Vitendo. Jaji  Mkuu amesema, amegundua changamoto hiyo baada ya kupata nafasi ya kukutana ana kwa ana na waombaji wa uwakili wapatao 824 kwa mujibu wa kifungu 8 (3) cha Sheria ya Mawakili.

Miongoni mwa mawakili hao 909  waliokubaliwa kupata uwakili saba ni majaji, aliyekuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Valentino Mlowola na  Msajili wa Mahakama ya Rufani John Kahyoza. 
Wengine ni  Balozi mstaafu na mwanadiplomasia  wa Umoja wa Mataifa, Tuvako Manongi Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Thomas Simba, maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Polisi, mapadre, mashekhe na watu wengine.
Akizungumza wakati hafla hiyo, Jaji Juma amesema,  lengo la kuwahoji lilikuwa ni kutaka kujiridhisha na ufahamu na matumizi ya lugha ya Kiingereza kwa mambo yanayozunguka sheria kwa Tanzania na dunia. 

"Changamoto ya kujieleza inatakiwa kufanyiwa kazi na mfumo wa elimu pamoja na Baraza la Sheria Tanzania chini ya Jaji Kiongozi.
"Mwalimu Nyerere aliwahi kutamka Kiingereza ni 'Kiswahili cha Dunia'.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...