Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) unaendesha mafunzo yakuwajengea uwezo wajasiriamali 1000 wa Mkoani Singida ikiwa ni hatua mojawapo yakuwawezesha kushiriki katika ujenzi wa uchumi kwa kufanya biashara katika mfumo rasmi.
Akizungumza mjini Singida wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo  leo mjini humo, Mkuu wa Wilaya hiyo Bw.Pascas Muragiri amesema kuwa  mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka ambapo Serikali inasisitiza wajasiriamali kufanya biashara katika mfumo rasmi ili waweze kukuza biashara zao na kuongeza tija.
“Mafunzo haya ni nyenzo muhimu kwa wajasiriamali wetu hapa Singida kwani yatawawezesha kuwa na uwezo wa kutambua na kuzingatia taratibu zote zinazosimamia biashara hali inayotoa fursa kwao kurasimisha biashara zao.” Alisisitiza Muragiri. Akifafanua amesema kuwa katika mafunzo hayo wajasiriamali hao watajifunza namna ya kutunza hesabu, Urasimishaji, taratibu za kupata leseni za biashara,umuhimu wa kutunza kumbukumbu za biashara na umuhimu wa bima ya afya.
Aliongeza kuwa wajasiriamali hao wanajukumu la kuzingatia yale watakayojifunza wakati wa mafunzo hayo na hivyo kuendana na dhamira ya Serikali kuwawezesha kukuza uwezo wa kufanya biashara baada ya kurasimisha biashara zao hali itakayowawezesha kupata mikopo katika taasisi za fedha ili kukuza mitaji yao na pia kuwezesha kukua kwa biashara katika mkoa huo na Taifa kwa ujumla.
  Mkuu wa Wilaya ya Singida Bw. Pascas Muragiri akizungumzia faida za kurasimisha Biashara kwa wajasiriamali wa mjini Singida wakati akifungua mafunzo kwa wajasiriamali zaidi ya 1000 wa mjini humo (hawapo pichani) yaliyolenga kuwajengea uwezo ili warasimishe Biashara zao, Mafunzo hayo yanaendeshwa na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) kwa kushirikina na Halmashauri ya Manispaa ya Singida.
 Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida Alhaji Gwae Mbua akisisitiza jambo kwa wajasiriamali zaidi ya 1000 wa mjini Singida (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kufungua mafunzo kwa wajasiriamali hao mjini humo mapema Novemba 10, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Singida Bw. Pascas Muragiri na Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Urasimishaji kutoka MKURABITA Bw. Japhet Werema.
 Sehemu ya Washiriki wa Mafunzo yakuwajengea uwezo wajasiriamali zaidi ya 1000 wa mjini Singida wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Wilaya ya Singida Bw. Pascas Muragiri wakati wa hafla yakufungua mafunzo hayo mjini humo Novemba 10, 2018.
 Mkuu wa Wilaya ya Singida Bw. Pascas Muragiri (katikati walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya washiriki na watoa mada wa mafunzo kwa wajasiriamali zaidi ya 1000 wa mjini humo yaliyolenga kuwajengea uwezo ili warasimishe Biashara zao, Mafunzo hayo yanaendeshwa na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) kwa kushirikina na Halmashauri ya Manispaa ya Singida.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...