*Ni baada ya kukiri makosa ya kutakatisha fedha, kuongoza genge la kuiba mafuta bomba la bandari

Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu mmiliki wa Kampuni ya mabasi ya Princes Muro Majid Kimaro kulipa faini ya Sh. milioni 115 au atatumimia kifungo cha miaka nane jela baada ya kukiri mashtaka yanayomkabili ya kutakatisha fedha na kuongoza genge la uhalifu ili kuiba mafuta katika bomba linalomilikiwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).

Pia Mahakama imeamuru gari aina ya Scania lenye namba za usajili T 856 ADH ambalo lilitumika kuiba mafuta hayo ambayo ni zaidi ya lita 26,875.25 ya dizeli na petroli litaifishwe na kuwa mali ya Serikali.

Hukuumu hiyo imesomwa leo Desemba 12, 2018 na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba na kuhukumiwa na jopo la mawakili likiongozwa na Wakili wa Serikali Wankyo Simon akisaidiana na Jackline Nyantori, Patrick Mwita

Alitoa Hukumu hiyo, Hakimu Simba amesema, Mahakama imemtia hatiani mshitakiwa kwa makosa mawili baada ya kukiri kutenda makosa hayo mwenyewe.

Akisoma adhabu, amesema, katika shitaka la kuongoza genge la uhalifu, Muro anahukumiwa kulipa faini ya Sh. milioni tano na iwapo akishindwa atatumimia kifungo cha miaka mitatu gerezani. Wakati katika shtaka la utakatishaji fedha, mshtakiwa ameamriwa kulipa faini ya Sh.milioni 110 au kutumikia kifungo cha miaka mitano gerezani.

Pichani mshtakiwa Majid Kimaro ambaye ni mmiliki wa Kampuni ya mabasi ya Princes Muro akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kufanikiwa kulipa faini ya Sh. Milioni 115 na kukwepa kutumikia kifungo cha miaka nane gerezani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...