Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

UKUAJI wa uchumi wa Taifa kutojionesha katika  kuongezeka kwa kipato cha kila mwananchi ni jambo la kawaida ambalo halimaanishi kuwa takwimu za ukuaji huo wa uchumi ni za kupikwa.

Hayo yameelezwa kwa Mkurugenzi wa Utafiti na Sera za Uchumi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Dk. Suleiman Missango alipokuwa akitoa mada katika semina kwa waandishi wa habari za uchumi na biashara
inayoendelea jijini Dodoma.

Akifafanua Dk Missango alisema kuwa takwimu za ukuaji wa uchumi zinatokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa jumla katika taifa ambapo mapato yake yanatofautiana katika kumwendea kila mmoja kutegemeana na shughuli za uzalishaji.

Akitoa mfano kuhusiana na suala hilo, alisema kuwa shughuli za uzalishaji za jamii moja zinaweza kuwa zimeongezeka kwa kuhesabu wastani wa ongezeko la uzalishaji, lakini haina maana kuwa kila mwanajamii atakuwa ameona ongezeko katika kipato chake, kutokana
na shughuli za kiuchumi alizonazo.

Katika siku za karibuni kumekuwa na malalamiko miongoni mwa wananchi wakihoji takwimu za ukuaji wa uchumi zinazoonekana kuimarika ilhali wananchi wengi wamekuwa hawana pesa. Uchumi wa Tanzania unakaridiwa kukua kwa kasi ya asilimia 7 kwa mwaka.Dk Missango alisema kuwa hali ya baadhi ya wananchi kupungukiwa fedha mifukoni inatokana na kupunguza matumizi yao ya kawaida na kuyaelekezwa katika matumizi ya maendeleo, ambapo athari za kushuka chini (trickledown effect) hupungua.
 Mkurugenzi wa Sera za Uchumi na Utafiti wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk. Suleiman Misango akifafanua kuhusu hali ya uchumi kwenye mafunzo ya waandishi wa habari za uchumi na biashara mjini Dodoma
Meneja wa Idara ya Itifaki na Uhusiano wa Umma wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Zaria Mbeo (kushoto), akijadiliana jambo na wakurugenzi wa Idara ya uchumi wa BoT, Tawi la Dodoma
 Mwenyekiti wa mafunzo ya waandishi wa habari za uchumi na fedha, Nurdin Selemani kutoka Azam Media, akijadiliana jambo na mtunza muda wa mafunzo hayo, Bakari Kimwanga kutoka Gazeti la Mtanzania Bakari Kimwanga (aliyekaa)
 Baadhi ya maofisa wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT) wakifuatilia mjadala wakati wa semina ya waandishi wa habari za uchumi na fedha inayoendelea mjini Dodoma.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...