Na Mwashungi Tahir - Maelezo Zanzibar

MWAKILISHI wa Jimbo la Magomeni Rashid Makame Shamsi amewaomba wananchi wa magomeni wandaras kuwa na mashirikiano na viongozi wao ili wanapopeleka huduma muhimu za maendeleo kwa jamii zipate ufumbuzi.

Hayo ameyasema huko Magomeni Wandaras wakati alipokuwa akikabidhi wananchi mipira ya maji katika shehia hiyo ikiwa anatimiza ahadi yake ili wananchi wa shehia hiyo waweze kupata huduma ya maji safi na salama kwa ukaribu na kupunguza masafa marefu yaliyokuwa yakiwakabili.

Amesema iwapo viongozi wa jimbo wanajitokeza kwa kuleta huduma za maendeleo inapaswa kuthamini na kuyafanyia kazi kwa moyo mmoja ili na wao waweze kufarijika zaidi na kuongeza kutatua changamoto nyengine zitazojitokeza .

Amesema wakati mliponichagua niliahidi kutatua changamoto na kuleta mambo ya maendeleo katika jimbo kati ya ahadi hizo ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma zote muhimu miongoni mwa hayo ni maji safi na salama hii ikiwa ilani ya Chama chetu cha Mapinduzi kuwajali wananchi wake katika pande zote.
Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Rashid Makame Shamsi akikabidhi Mipira ya maji kwa Mzee wa mtaa Azizi Mbarouk Omar ( Kushoto) huko Shehia ya Magomeni Wandaras Mjini Unguja.Picha na Mwashungi Tahir – Habari Maelezo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...