THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Mwenyekiti Tume ya Madini, atatua mgogoro sugu wa madini, Nzega

Na Greyson Mwase, Nzega.

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula leo tarehe 06 Desemba 2018 ametatua mgogoro uliodumu kwa muda mrefu kati ya vikundi viwili vilivyokuwa vinajishughulisha na shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu katika eneo la Mwamikola lililopo Wilayani Nzega mkoani Tabora.

Vikundi hivyo ni pamoja na kikundi cha Mwaguguli Mining Society na kikundi cha Mwamikola Gold Mining Society ambapo mgogoro wao ulitokana na mwingiliano wa maombi ya leseni za uchimbaji mdogo wa madini.

Profesa Kikula aliyekuwa Wilayani Nzega kwa ajili ya kutatua mgogoro huo aliambatana na watendaji mbalimbali ikiwa ni pamoja na Kamishna kutoka Tume ya Madini, Dk. Athanas Macheyeki, Meneja wa Leseni kutoka Tume ya Madini, Mhandisi Zephania Maduhu na Mwanasheria kutoka Tume ya Madini, Hadija Ramadhani.

Wengine waliokuwepo katika ziara hiyo ni pamoja na Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Tabora, Mayigi Makolobela, Katibu Tawala wa Wilaya ya Nzega, Onesmo Kisoka, Vyombo vya Ulinzi na Usalama vya Wilaya pamoja na waandishi wa habari.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula (katikati kushoto) na Kamishna kutoka Tume ya Madini, Dk. Athanas Macheyeki wakikagua moja ya mashimo ya kuchimba dhahabu yaliyopo katika kijiji cha Mwamikola katika Wilaya ya Nzega mkoani Tabora tarehe 06 Desemba, 2018
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula (kushoto) akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu  katika kijiji cha Mwamikola  kilichopo katika Wilaya ya Nzega mkoani Tabora
Mmiliki wa eneo lililopo katika kijiji cha Mwamikola kilichopo katika Wilaya ya Nzega mkoani Tabora, Rashid Kavula ( kushoto) pamoja na Katibu wa Kikundi cha wachimbaji wa madini ya dhahabu kilichokuwa kinaendesha shughuli zake za madini katika eneo hilo cha Mwaguguli Mining Society, Nyansaho Sumar (kulia) wakishikana mikono kama ishara ya kumaliza mgogoro baina yao kwenye mkutano wa wachimbaji wadogo wa madini uliofanyika katika kijiji hicho.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula ( wa nne kutoka kulia mbele), Kamishna kutoka Tume ya Madini Dk. Athanas Macheyeki ( wa tatu kutoka kulia mbele) na Katibu Tawala wa Wilaya ya Nzega, Onesmo Kisoka ( wa tano kutoka kulia mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya watendaji kutoka Tume ya Madini na wachimbaji wa madini katika eneo la Mwamikola lililopo Wilayani Nzega mkoani Tabora mara baada ya kutatua mgogoro huo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA