Na Editha Shija, Tabora

MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega mkoani Tabora Kiwele Michael Bundala ametoa onyoa kali kwa watendaji wa Vijiji na Kata watakaobainika kutafuna fedha za mapato wanayokusanya kutoka katika vyanzo mbalimbali katika halmashauri hiyo.

Ametoa onyo hilo jana wilayani hapa baada ya kutoridhishwa na utendaji wa baadhi ya watumishi wa halmashauri hiyo kutowasilisha fedha za mapato kwa wakati ambapo amesema halmashauri inakusanya fedha nyingi kutoka katika vyanzo vyake mbalimbali lakini nyingi zinaingia mifukoni mwa baadhi ya watu.

Pia amesisitiza kuwa watendaji wote wanapaswa kuhakikisha fedha zote zinakusanywa katika maeneo yao na kuletwa kama zilivyo na kwamba kuanzia sasa Mtendaji yeyote atakayebainika kutafuna fedha za mapato au kujihusisha na vitendo vya rushwa atachukuliwa hatua za kinidhamu pamoja na kutimuliwa mara moja.

Amewasisitiza 'kuwa waadilifu na kutekeleza majukumu yao kwa kufuata kanuni,taratibu,na sheria huku akionya kuwa Serikali haina fedha za kuhamisha mtumishi mzembe anayeshindwa kutekeleza majukumu yake. Hata hivyo Mwenyekiti huyo amewataka madiwani wa kata zote kufuatilia kwa ukaribu watendaji wao na kuhakilisha fedha zote zinazokusanywa na kuwasilishwa ipasavyo.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...