NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof Kitila Mkumbo kumtafutia kazi nyingine Mhandisi wa maji Wilaya ya Pangani Novath Wilson kutokana na kushindwa kusimamia ipasavyo miradi ya maji wilayani humo na kupelekea wananchi kushindwa kupata huduma hiyo muhimu kwa wakati.

Ametoa agizo hilo wakati akiwa wilayani Pangani ikiwa ni ziara yake ya siku mbili mkoani Tanga alipotembelea miradi mbalimbali ya maji inayotekelezwa wilayani humo na kutokuridhishwa nayo kutokana na utekelezaji wake kuwa chini ya kiwango hatua iliyomlazimu kuzivunja baadhi ya kamati za usimamizi wa maji ambapo ziara hiyo alianzia wilayani Muheza

Licha ya mhandisi huyo kutoa sababu mbalimbali ya baadhi ya miradi kukwama kutoa maji lakini Naibu Waziri huyo alionyeshwa kutokuridhishwa na majibu hayo kutokana na baadhi ya maelekezo aliyokuwa akimpa ili kuweza kukabiliana na changamoto juu ya miradi hiyo.

“Nimekuita marangapi Wizarani tena nikakukutanisha na viongozi wengi labda watakusaidia na kila mara nakupigia simu lakini bado unaonekana si mtendaji wa kazi sasa nitamwambia Katibu Mkuu wetu akutafutie kazi sehemu nyingine lakini sio hapa Pangani”Alisema Aweso.

NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso wa kwanza kulia akikagua mabomba yatakayotoa maji eneo la Kilapula ambayo yatapeleka maji wilayani Muheza  kutoka Pongwe Jijini Tanga wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani Tanga kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maji kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Maji Tanga Uwasa Mhandisi Jofrey Gerald
NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso kushoto akiwa na Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia wakati wa ziara yake
NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso akikagua moja ya miundombinu ya maji wilayani Pangani
Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akipanda juu kuangalia tanki ya kuhifadhiwa maji eneo la Ngomeni wilayani Muheza ambapo mradi huo unatoa maji katika eneo la Pongwe Jijini Tanga na kuyapeleka wilayani humo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...