RS TABORA

MKANDARASI wa Ujenzi wa Ofisi za Halmashauri ya Mji Nzega wenye thamani ya bilioni 4.8 ametakiwa kuhakikisha mradi huo unakamilika katika kipindi ambacho kimekubalika katika mkataba.

Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali (OR TAMISEMI) Mwita Waitara wakati wa ziara yake wilayani Nzega.

Alisema Wakandarasi wanaopatiwa fursa ya kujenga miradi ya Serikali ikiwemo ile ya Halmashauri ni vema wakajitahidi kuhakikisha wanaitekeleza kwa kiwango cha hali ya juu ili iweze kudumu kwa muda mrefu.

Akijibu hoja za Wakala wa Majengo Tanzania(TBA) kuchelewesha miradi mingi mkoani Tabora ikiwemo ukarabati wa Shule Kongwe ya Milambo na huo wa ujenzi wa Ofisi hizo alisema atajitahidi kulifikisha katika Wizara inayoisimamia Wakala hiyo ili watekeleze miradi yao kwa wakati.

Alisema TBA kama sehemu ya Serikali ni lazima wabadilike na kuharakisha utekelezaji wa miradi wanayopewa kusimamia ili kutosababishia kuongezeka kwa gharama kutokana na mradi kuchelewa kuanza. Awali Mahandisi wa Halmashauri ya Mji Nzega Mwita Said alisema ujenzi wa Ofisi hizo ulioanza Mei mwaka huu unatarajia kukamilika Novemba mwakani .

Alisema hadi hivi wameshapokea bilioni 2 na wamemlipa Mkandarasi ambaye ni Mzinga Holding milioni 700 na Msimamizi ambaye ni TBA milioni 200. Said alisema mradi huo uko katika hatua ya Msingi ambao umekumbana na matatizo ya kuwepo kwa mvua, ardhi kuwa na mwamba na upungufu wa vibarua unasababisha kazi kwenda polepole.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...