Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza kufanyika kwa uchaguzi mdogo katika Jimbo la Temeke, Mkoani Dar es Salaam na kwenye Kata 46 za Tanzania Bara.

Akitangaza kufanyika kwa uchaguzi huo Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji (Rufaa), Semistocles Kaijage amesema kuwa uchaguzi huo utafanyika Januari 19 mwaka 2019 na fomu za uteuzi wa wagombea zitatolewa kuanzia tarehe 14 hadi tarehe 20 Desemba 2018.

"Uteuzi wa Wagombea utafanyika tarehe 20 Desemba, mwaka huu. Kampeni za Uchaguzi zitafanyika kati ya tarehe 21 Desemba, hadi tarehe 18 Januari, mwaka 2019 na siku ya uchaguzi itakuwa ni tarehe 19 Januari mwaka 2019,” amesema Jaji Kaijage.Jaji Kaijage amebainisha kuwa Tume imetangaza uwepo wa nafasi wazi ya Ubunge kwenye Jimbo la Temeke baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai juu ya uwepo wa nafasi wazi ya Ubunge katika jimbo hilo.

Amesema kuwa Tume ilipokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye kwa kuzingatia kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, aliitarifu Tume uwepo wa nafasi wazi ya Mbunge wa Jimbo la Temeke katika Halmashauri ya Wilaya ya Temeke Mkoani Dar es Salaam kufuatia Kujiuzulu uanachama wa Chama Wananchi CUF kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Maulid Said Abdllha Mtolea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...