Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

SHIRIKA la taifa la hifadhi ya jamii (NSSF) limeshiriki katika maonesho ya tatu ya bidhaa za viwanda vya Tanzania yaliyozinduliwa rasmi leo katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es salaam kwa kutoa huduma kwa wajasiriamali ikiwa ni mchakato kwa kukamilisha azma ya ujenzi wa Tanzania ya viwanda.

Akizungumza na blogu ya jamii Afisa mwandamizi kitengo cha sekta isiyo rasmi  (NSSF) Abas Cothema amesema kuwa, wameungana na shirika la kuhudumia viwanda vidogo vidogo nchini (SIDO)  katika maonesho hayo ya bidhaa za viwanda zinazozalishwa nchini ikiwa ni  kuunga mkono  jitihada za Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais Dkt. John Magufuli iliyodhamiria kujenga Tanzania ya viwanda.

Amesema kuwa NSSF imeshiriki maonesho hayo ili kuhakikisha wanawapatia hifadhi ya jamii wajasiriamali ili waweze kukingwa dhidi ya majanga yanayosababisha  upotevu wa kipato na kuwapa pensheni ya uzeeni, pensheni ya ulemavu, pensheni ya  urithi na bima ya afya ambazo vyote hivyo ni muhimu katika ujenzi wa Tanzania mpya ya viwanda.

Cothema amesema kuwa mwanachama akishiriki kwa kuchangia ada ya kima cha shilingi 20,000/= kwa muda wa miezi mitatu atapata bima yeye na wategemezi wake wanne yaani watoto wanne walio na umri chini ya miaka 18 na watoto wanaosoma walio chini ya miaka 21 pamoja na mtegemezi wake na malengo ya kufanya hivyo ni kumkinga mwanachama na majanga ya maradhi na magonjwa ili aweze kuendelea na shughuli za ujenzi wa uchumi ambao Serikali umejizatiti kuufikia pia kufanya hivyo ni kusaidia serikali katika kutoa huduma kwa wananchi wake.

Ameeleza kuwa NSSF wana miradi mbalimbali ya kiuchumi ambayo imelenga kuwasaidia wananchi wa hali zote ikiwa ni pamoja na  viwanja vilivyo katika maeneo ya kiluvya na visiga ambavyo hupatikana kwa gharama ambayo kila mwananchi anaweza kumudu hata kwa mkopo au kwa malipo ya muda mrefu.

Pia amesema kuwa wanashirikiana bega kwa bega na serikali na wadau mbalimbali katika kuhakikisha azma ya ujenzi wa Tanzania ya  viwanda na kufikia uchumi wa kati mwaka 2025 inafikiwa.
Naibu wa Viwanda Biashara na Uwekezaji,Mhandisi Stella Manyanya aliyeambatana na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara,Edwin   Rutageruka, akisalimiana na mmoja wa afisa wakitego cha sekta isyo rasmi wa (NSSF) wakati alipotembelea Shirika la Taifa la hifadhi ya jamii (NSSF)  leo jijini Dar es Salaam katika  maonyesho Tatu ya Bidhaa za Viwanda.
Naibu Waziri wa Viwanda biashara na uwekezaji,Mhandisi Stella Manyanya (kushoto) akisisitiza jambo kwa,Abbas Cothema Ofisa Matekelezo kutoka Kitengo cha Hiari-NSSF alipotembelea banda la NSSF ndani ya maonyesho ya tatu ya bidhaa za wiwanda vya hapa nchini yaliyo funguliwa leo jijini Dar es Salaam.
Ofisa Matekelezo kutoka Kitengo cha Hiari-NSSF    Abbas Cothema akizungumza na Michuzi blog  katika maonyesho ya tatu ya bidhaa za wiwanda vya hapa nchini yaliyo funguliwa leo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...