Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila

Na Mwandishi Wetu, Mbeya

MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amewataka wamachinga mkoani humu kujiendeleza na kuwa wafanyabiashara badala ya kupenda kuendelea kuwa wamachinga. Chalamila ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na HabariLeo kutolea ufafanuzi uamuzi wake wa kuwataka wamachinga waondoke kwenye maeneo yasiyokuwa rasmi.

Aliwataka wamachinga hao kutambua kuwa umachinga wao unapaswa kuwa kwa miaka mitatu na zaidi ya hapo wanapaswa kuanza kulipa kodi zote stahiki. 

Alisema.“Kuna mijadala inaendelea kwenye mitandao ya kijamii kuwa nimewafukuza wamachinga mkoani kwangu sasa swali ni kuwa kama wao ni wapangaji unawafukuzaje, maana wanasema wamachinga wamefukuzwa, 

Ni vema wakafahamu kuwa umachinga haupaswi kuwa sifa ya kudumu, machinga sahihi inatakiwa uwe mabadiliko ya kuelekea kuwa mfanyabiashara wa kati katika eneo moja tulivu katika maduka.“ 

Pia Mkuu huyo wa Mkoa aliitaka ofisi ya Mamlaka ya Mapato (TRA) mkoani humo kufuatilia ukuaji wa biashara za wamachinga hao ikiwa ni pamoja na kuwapatia elimu ya maarifa na ujuzi za biashara. 

Lakini pia alisisitiza kuwa anawapenda na anata kuona wananufaika na hivyo katika kutimiza adhma hiyo aliwataka kuwa na Saccos ya pamoja itakayowasaidia kupata mikopo kwa bei nafuu na hivyo kujipatia faida.

Alisema“Rais Dk John Magufuli anawapenda Machinga wote nchin, na amekuwa akitutaka viongozi kutowabughudhii na hivyo siye mkoani hapa tunaendelea kuzingatia maelekezo ya Mh Rais kwa utaratibu maalumu"

Aliwataka, wamachinga wote kutumia vema misamaha ya rais yenye nia njema kwa kufuata utaratibu na kukua katika biashara.

“Tuwafundihse Machinga kulipa kodi hata kama ni kidogo, ili kesho wakiwa wafanyabiashara wa Kati au wakubwa wawe tayari wamejenga utamaduni wa kulipa kodi kwa hiari" alisema Rc Chalamila.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...