Kama Real Madrid walihitaji kujua ni nani wa kumuhofia kwenye fainali za mwaka huu za Klabu bingwa ya Dunia, basi majibu yalipatikana Jumapili iliyopita ambapo miamba kutoka Amerika ya Kusini, River Plate na Boca Juniors waliumana katika dimba la Santiago Bernabeu na Rive Plate kuibuka vinara. Bingwa wa Ulaya na wa Amerika ya Kusini huingia katika hatua ya nusu fainali na mara nyingi (mara 10 kati ya fainali 13 zilizopita) hukutana fainali.

Real Madrid wameshinda fainali mbili zilizopita za Klabu Bingwa ya Dunia na baada ya kumjua mpinzani wao kutoka Amerika ya Kusini wikendi iliyopita watakuwa wanajipanga kushinda kwa mara ya tatu mfululizo kama walivyofanya kwenye Kombe la Klabu bingwa Ulaya. River Plate walishinda mchezo wa pili wa fainali ya CONMEBOL ambao ulichezwa jijini Madrid katika uwanja wa nyumbani wa klabu ya Real Madrid, Santiago Bernabeu baada ya mechi hiyo kuahirishwa mara mbili jijini Buenos Aires, mara ya kwanza kufuatia mvua kubwa na mara ya pili basi la Boca Juniors kushambuliwa na mashabiki wa River Plate.

Wapenzi wa soka barani Africa wataweza kutazama michuano hii kupitia chaneli za michezo za StarTimes ambao ndio warushaji rasmi wa michuano hii kwa ukanda wa Africa. Beki wa kati wa Klabu ya Real Madrid Raphael Varane ambaye mwaka huu alishinda Kombe la Dunia na timu ya taifa ya Ufaransa tayari ameshacheza fainali 3 za Klabu bingwa ya Dunia na kushinda zote, aliiambia tovuti ya timu hiyo kwamba wanakwenda Abu Dhabi kushinda tena.

“Tunapenda kuendelea kuweka historia, tuna shauku kubwa kwa sababu sio rahisi kufika hatua hii, unahitaji kushinda ligi ya mabingwa “Hakuna timu ambayo imewahi kushinda mara tatu Kombe hili na sisi tunataka kuweka historia mpya. Tunafahamu ni ngumu lakini lakini tunayo njaa na ari ya kushinda” alisema Varane. Kwa mwaka huu Klabu bingwa ya dunia itachezwa katika Falme za Kiarabu kuanzia tar 12 hadi 22 Disemba. Mchezo wa kwanza unawakutanisha Al Anin ya nchini humo na Team Wellington ya New Zealand saa 12:30 jioni na utarushwa moja kwa moja kupitia ST World Football.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...